The House of Favourite Newspapers

Kadja Nito: Kwenye Ndoa Nafuata Upendo Siyo Pesa

kadja

Mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Khadija Said ‘Kadja Nito’ anayetarajiwa kufunga ndoa Jumamosi ijayo amefunguka kuwa kwa mumewe mtarajiwa, anafuata upendo wa kweli siyo pesa kama mastaa wengine wanavyofanya.

Akistorisha na Wikienda, Kadja alifunguka kuwa, mumewe huyo siyo pedeshee kama wanavyodhani baadhi ya mastaa na kuongeza kuwa ndoa yake itakuwa simpo kwani hata mastaa hawatakuwepo na anachoangalia yeye si ustaa bali kukamilisha ahadi ya Mungu.

KADJA NITO (4)

“Mastaa wengi hawaolewi kwa sababu wanaangalia mwanaume mwenye pesa, nimeamua kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya upendo na siyo pesa,” alisema Kadja.
Kadja amefanyiwa kibao kata jana na sasa anasubiri ndoa itakayofungwa kwenye Kanisa la Ufufuo la Nabii Bendera.

Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda

Comments are closed.