The House of Favourite Newspapers

Kifua Kikuu (Tuberculosis)

0

TB-2.jpgKIFUA kikuu ni moja ya magonjwa  yanayochukua nafasi  za juu kati ya magonjwa  kumi yanayotibika, lakini husababisha vifo  kwa wingi katika jamii nyingi duniani.

Uchunguzi wa hivi karibuni umebaini kupatikana kwa jamii ya vijidudu vinavyokadiriwa kufika 100 ambavyo ni jamii ya wadudu wa kifua kikuu maarufu kama TB.

Vijidudu hivyo hujulikana kwa kitaalamu kama ifuatavyo; M.tuberculosis, M.leprae ambavyo husababisha ukoma M.cevicum comlex, M.kansasii, M.fortuitum, M.chelonae na M.abscessus.

Wadudu wa kifua kikuu hujulikana kama Gram Positive Acid-fast Bacilli. Ugonjwa wa kifua kikuu hutokea kwa njia mbili, moja hujulikana kama Primary Infection  mtu kuambukizwa vijidudu hivyo na kusababisha ugonjwa .

Njia nyingine hujulikana kama Dissemination hii hutokea baada ya  mtu aliyeingiwa na wadudu wa TB lakini kwa kuwa anakinga ya kutosha vijidudu ‘husinzia’ na kupooza hivyo haviwezi kuleta ugonjwa lakini mara kinga ikishuka kama mgonjwa wa Ukimwi, vile vijidudu huchachamaa  na kusababisha ugonjwa.

DALILI: Kikohozi kikavu cha mfululizo cha wiki mbili ambacho hakisikii dawa za kuua vijidudu Antibiotic, Kutoka jasho usiku, ambalo linalowanisha hadi nguo ulizolalia, homa hasa usiku, kukonda na kikohozi cha damu.

Tiba ya ukweli inapatikana, kinga yenye uhakika pia hupatikana lakini tatizo ni watu kutowahi kwenda hospitali kwa vipimo na dawa sahihi.

Leave A Reply