The House of Favourite Newspapers

King Kiki: Linex, Bella wapo juu

0

Christian Bella & Malaika Band - AmerudiChristian Bella

Na Elvan Stambuli, Risasi Jumamosi
Ngwiji wa Muziki wa Dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ amesema wanamuziki wawili mahiri nchini, Linex na Christian Bella wapo juu kutokana na uwezo wao wa kuimba.

king kikiiNgwiji wa Muziki wa Dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’.

Akizungumza katika kipindi maalum cha Mboni Show hivi karibuni, King Kiki alisema: “Kwa kweli vijana hao wanaweza, wanatunga na kuimba vizuri sana muziki.”Akizungumzia mipango yake ya baadaye, Kiki alisema bado anahitaji wafadhili kwa sababu anajiamini kwamba ana uwezo wa kufanya mambo makubwa kimuziki.

“Wafadhili wapo lakini wanaangalia upande mmoja tu wa mchezo wa mpira wa miguu. Naamini kwenye muziki wa dansi, nikipata wafadhili nitaonesha maajabu kwa sababu kila mtu anajua kwamba licha ya ujuzi, mtu lazima uwe na fedha kutekeleza miradi,” alisema King Kiki.

Leave A Reply