The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa Upinzani, Azuiwa Kwenda Kupokea Tuzo

0

KIONGOZI  wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,  amezuiwa kusafiri kwenda Hispania kupokea Tuzo ya Haki za Binadamu.

 

“Niliandika barua kwa Waziri wa Sheria kuomba kibali cha kusafiri kwenda nje, lakini, kama kawaida, waziri hakuijibu.” alisema Ingabire akizungumza na shirika la habari la The Associated Press.

 

Hata hivyo, watoto wake waliipokea tuzo hiyo kwa niaba yake Alhamisi iliyopita huko Hispania.

 

Mpinzani huyo aliendelea kusema kwamba mnamo mwezi Mei mwaka huu, serikali ilitupilia mbali ombi lake la kutaka kwenda Ujerumani kwa ajili ya mkutano.

 

Ingabire alikaa miaka 16 ukimbizini huko Uholanzi na alirejea Rwanda na kuanzisha chama cha upinzani  mwaka 2010 lakini alitupwa jela kabla ya uchaguzi wa nafasi ya urais.

 

Rais Paul Kagame mwaka jana alimsamehe baada ya kutumikia miaka minane ya kifungo cha miaka 15 kutokana na mashtaka ya ugaidi ambayo Ingabire alisema yalibuniwa kwa nia za kisiasa.

Leave A Reply