The House of Favourite Newspapers

Kisa kubemendwa na Baby J… Mo Music atokwa povu

1

mo musicMAYASA MARIWATA

MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amejikuta akitokwa povu baada ya kuandamwa kuwa mwandani wake wa sasa ‘Baby J’ anambemenda sababu wamepishana kwa zaidi ya miaka sita.

Showbiz: Mambo Mo Music upo?

Mo Music: Kama kawa maisha yanasonga!

Showbiz: Vipi mubebezi wako, yupo?

Mo Music: Mubebezi, yupi tena?

Showbiz: Si yule aliyekuzidi umri, yule ambaye watu wanadai eti anakubembenda kakuacha zaidi ya miaka sita?

Mo Music: Embu sikia, hao wanaosema ananibembenda wao wamejipima wapoje? Watanichaguliaje mtu ninayevutiwa naye?

Showbiz: Hivi ni kweli amekuzidi umri?

Mo Music: Anizidi, asinizidi hiyo haiwahusu!

Showbiz: Vipi muziki sasa, sababu wote mnaimba, mna mpango wowote labda wa kolabo?

Mo Music: Sitaki kulizungumzia lolote, hiyo mipango kama ipo nitasema hapo baa-daye, tena uwa-ambie hao wanao-chonga bora wakae kimya tu… (akakata simu)

1 Comment
  1. Global Publishers says

    Someni Zaid Habari zetu

Leave A Reply