The House of Favourite Newspapers

Kisa kuboronga Kiingereza Mashabiki wamtetea Barakah The Prince

0

baraka prince (2)Barakah The  Prince

HIVI karibuni msanii anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Barakah The  Prince ametengeneza vichwa vya stori za burudani kwenye media mbalimbali kufuatia kuvuja kwa video inayomuonesha akishindwa kuzungumza Lugha ya Kiingereza wakati anahojiwa na Kituo cha MTV.

Video hiyo ilianza kuvuja kupitia kwenye Ukurasa wa Instagram wa kituo hicho, inayomuonesha mtangazaji wa MTV akimuuliza maswali Barakah ambapo kabla ya kujibu mpenzi wake Najma Dattan ‘Naj’ aliyekuwa naye alikuwa akidakia na kumtafsiria kisha baada ya yeye kujibu alimuelezea pia mtangazaji huyo.

barakahBarakah na mpenzi wake, Najma Dattan ‘Naj’

Baada ya video hiyo kusambaa, watu wengi waliyojitokeza kukomenti chini ya video hiyo walionekana kumtetea Barakah juu ya mtazamo wa wachache ambao walikuwa wanamponda, zaidi waliiponda elimu ya Tanzania waliyodai ni duni na haimpi mtu msingi mzuri wa kuzungumza lugha hiyo ya kimataifa tangu akiwa shule za awali.

“Hili si jambo la kumcheka jamani, nyie wenyewe mnafahamu kuwa elimu yetu ni magumashi, hata hivyo yeye si wa kwanza, wapo wasanii wengi tena wakubwa wamewahi kuboronga ngeli,” alikoment mtu mmoja.

Hata hivyo, kwenye komenti zingine, mashabiki hao walimshauri Barakah ambaye yuko Afrika Kusini kwa ajili ya kushuti video ya wimbo wake mpya na kufanya ziara kwenye media mbalimbali, kuhakikisha anaifahamu lugha hiyo ili aweze kukabiliana na changamoto hiyo.

Leave A Reply