The House of Favourite Newspapers

Kisa Okwi, Kagere, Simba yatikisa Afrika

KAULI ya bilionea wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ ya kuifanya klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu kubwa Afrika, imeanza kutimia baada ya wachezaji wake wawili Meddie Kagere na Emmanuel Okwi kutikisa Afrika.

 

Wawili hao wametikisa Afrika baada ya kuwemo kwenye orodha ya majina ya wachezaji ambao wanawania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ndani ya Afrika.

 

Kagere na Okwi wametajwa katika orodha hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) baada ya kuwa na mafanikio makubwa kwa msimu uliopita wakiifikisha klabu hiyo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kutajwa kwa wachezaji hao kuwania tuzo hiyo kumetengeneza rekodi kwa Simba kwa kuwa klabu pekee ya Ukanda wa Afrika Mashariki kutoa wachezaji wawili wanaowania tuzo hiyo lakini wakiwa miongoni mwa timu ambazo zimetoa wachezaji wawili katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Nchi hizo ni Afrika Kusini ina wawili, DR Congo ina watatu na Tanzania ina wawili.

 

Orodha kamili ipo hivi; Denis Ferjani Sassi (Tunisia & Zamalek), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Anice Badri (Tunisia & Esperance), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns) na Emmanuel Okwi (Uganda & Simba/Al Ittihad).

 

Wengine ni Ferjani Sassi (Tunisia & Zamalek), Fousseny Coulibaly (Ivory Coast & Esperance), Franck Kom (Cameroon & Esperance), Herenilson (Angola & Petro de Luanda), Ismail El Haddad (Morocco & Wydad Casablanca) na Jean Marc Makusu (DR Congo & AS Vita/ RS Berkane), Kodjo Fo Doh Laba (Togo & RS Berkane / Al Ain) na Mahmoud Alaa (Misri & Zamalek).

 

Pia wapo Meschack Elia (DR Congo & TP Mazembe/ FC Anderlecht), Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance), Tarek Hamed (Misri & Zamalek), Themba Zwane (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns), Trésor Mputu (DR Congo & TP Mazembe), Walid El Karti (Morocco & Wydad Casablanca) na Youcef Belaïli (Algeria & Esperance / Ahli Jeddah).

Comments are closed.