Kisutu: Kesi ya Aliyemchoma Mkewe kwa Magunia ya Mkaa

MAPEMA leo Jumatatu, Desemba 2, 2019, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara Hamis Said (38) umedai kuwa jarada bado lipo kwenye hatua ya mwisho ya uchapaji.

 

Hayo yamesemwa na wakili wa Serikali, Tully Helela mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika.

 

Helela amedai kuwa jarada lipo kwenye hatua ya uchapishaji hivyo anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

 

Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 16 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

 

Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


Loading...

Toa comment