The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Kocha Mkuu wa Yanga Awaaga Wachezaji na Benchi la Ufundi

pluijmHATIMAYE ikiwa ni siku moja baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans, Hans van Pluijm aandike barua ya kujiuzulu nafasi yake hiyo, baada ya kusikia kuwa kuna kocha kutoka Zesco United ya Zambia, George Lwandamina amekuja tayari Tanzania kuchukua nafasi yake, leo Oktoba 25 amewaaga rasmi wachezaji wake na benchi la ufundi.

Hans amewaaga wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi katika mazoezi ya leo asubuhi yaliofanyika katika uwanja wa Polisi Kilwa Road, kocha Hans anaondoka Yanga akiwa kaipa mafanikio makubwa ikiwemo kukushiriki hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, hatua ambayo Yanga wana miaka mingi toka waifikie.

Comments are closed.