The House of Favourite Newspapers

Kocha Mzambia Asaini Miaka 2 Yanga Kuchukua Mikoba ya Pluijm

lwandamina-2Kwa mujibu wa kituo cha redio E-FM, mtangazaji Maulid Kitenge ametangaza Kocha wa Klabu ya Zesco United, George Lwandamina amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa klabu ya Jangwani, Young Africans ‘Yanga’.
 
Hatua hii imefikiwa baada ya Yanga kutokuwa na matokeo yasiyoridhisha tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi mwaka huu.
Kocha George Lwandamina raia wa Zambia, yuko jijini Dar es Salaam.
 
Taarifa zimeeleza kwamba kocha huyo alitua jama mchana na kuwekwa katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam, Yanga wakitaka kufanya siri kubwa.
 
Kamati ya Ufundi ya Yanga, imempendekeza kocha huyo kutua nchini na kuinoa Yanga badala ya Kocha Hans van der Pluijm.
 
Hata hivyo, taarifa nyingine zimeeleza kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya Pluijm ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga.
 
Bado kumekuwa na mkanganyiko kuhusiana na kocha huyo kwa kuwa Yanga wamefanya ni siri kubwa.
 
Lakini habari za uhakika zimeeleza, tayari Yanga wamemalizana naye licha ya kuwa wanafanya siri kubwa kuhusiana naye.
 
“Kila kitu kimemalizika, kocha yuko Dar es Salaam, mambo yanakwenda safi kabisa. Lakini vuteni subira,” alisema mpasha taarifa.
 
Lwandami alikuwa kocha bora wa Zambia msimu wa 2014-15, pia aliwahi kuinoa Zesco ya Zambia kwa mafanikio makubwa, pia timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo.

Comments are closed.