The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm Ajiuzulu

PLUIJMKITAMBIIkiwa ni takribani wiki mbili tangu kuanza kusambaa kwa taarifa kuhusu hatma ya Kocha Mkuu wa Klabu ya Dar es Salaam Young Africans, Hans van Pluijm kuwa anakaribia kufutwa kazi na nafasi yake kurithiwa na kocha wa Zesco United George Lwandamina.

Jioni ya jana Oktoba 24, 2016 taarifa za kujiuzulu kocha huyo zimesambaa katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakishangazwa na maamuzi ya kocha huyo kutangaza kujiuzulu,Hans amejiuzulu kufuatia kusikia ujio wa kocha wa Zesco United George Lwandamina ambaye inaaminika amekuja kuchukua nafasi yake.

Akihojiwa na wanahabari jana kwa njia ya simu, kocha Hans van Pluijm amethibitisha kuwa ameuandikia barua ya kuomba kujiuzulu uongozi wa klabu ya Yanga na sasa anasubili majibu ya barua hiyo kutoka kwa viongozi hao.

Inadaiwa kuwa kilichosababisha viongozi wa Yanga kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans ni kutokana na kukataa kumrudisha kikosini Mrisho Ngassa aliyekuwa amevunja mkataba na Free State ya Afrika Kusini, Hans aliona hakuna haja ya kumrudisha Ngassa wakati kuna Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Simon Msuva.

Comments are closed.