The House of Favourite Newspapers

Kwa ninayoyaona, sitamani ndoa -Mary Mawigi

0

Mary Mawigi HAMIDA HASSAN, IJUMAA

MSANII wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi amesema kuwa tofauti na wanawake wengine wanaotamani ndoa, yeye hafi kirii kabisa suala hilo kutokana na jinsi anavyoona baadhi ya wanawake wanavyolia na kujuta kuolewa.

Mary Mawigi1Akipiga stori na Ijumaa, Mary alisema kuwa huenda watu wakamshangaa kwa kusema hivyo lakini ndiyo ukweli kwani idadi kubwa ya wanawake hawana furaha ya ndoa kutokana na sarakasi zilizomo ndani yake, hivyo yeye atabaki kuwa singo.

“Wapo marafiki zangu ambao walililia sana ndoa, hatimaye wakaolewa lakini sasa hivi wanatamani kutoka kutokana na kile wanachokiona, mateso na manyanyaso vinatawala, mimi ndoa noo kwa kweli,” alisema Mary.

Leave A Reply