Lamine Moro, Balinya na Molinga Wadaiwa Kuachana na Yanga
TAARIFA zilizoibuka kwa kasi leo Desemba 7, 2019, kupitia mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa wachezaji watatu wa Yanga ambao ni wa kimataifa, wameamua kuandika barua ya kuachana na klabu hiyo.
Wachezaji hao ni Juma Balinya ambaye anatokea Uganda, Lamine Moro kutoka Ghana na David Molinga maarufu kama Falcao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Inaelezwa wachezaji hao wameamua kuandika barua hizo wakiomba kuondoka kutokana na kutolipwa stahiki zao.
Taarifa za ndani zinasema Moro hajalipwa mshahara wa miezi mitatu pamoja na Molinga na Balinya ambaye pia anadai stahiki zake.
Msemaji wa Klabu wa Yanga, Hassan Bumbuli, alipopigiwa simu ya mtandao huu (Global Publishers) alisema hakuwa ofisini kwa siku ya tatu akielekeza kutafutwa kwa Katibu Mkuu wa Yanga.
Endelea kuwa nasi ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hili.