The House of Favourite Newspapers

Maajabu ya Programu Inayookoa Maisha ya Watu

POLISI nchini Uingereza wametaka kila mtu kupakua programu-tumishi ya simu ya mkononi wakidai kuwa programu hiyo imeshaokoa baadhi ya maisha ya watu. Je,programu hiyo ni ipi na inafanya kazi vipi?

 

‘Kicked. Converged. Soccer’ yaani Imepigwa, Imegeuzwa, Soka. Maneno hayo matatu ambayo yamechaguliwa bila kuwa na mpangilio yaliweza kuokoa maisha ya Jess Tinsley na rafiki zake baada ya kupotea kwenye msitu wakati wa usiku. Vijana hao walipotea na kutojua wanaweza kujiokoa vipi.

 

“Nilipopiga simu ya dharura, jambo nililoambiwa kufanya ni kupakua programu ya ‘what3words’, nilikuwa sijawahi kuisikia kabla ya hapo, baada ya dakika chache, polisi walijibu kwa kutuuliza ni wapi tulipo,” Bi. Tinsley alisema.

“Nilimwambia kila mtu ninayemjua kupakua programu hii kwa sababu hawawezi kujua lini wanaweza kupotea na kuhitaji huduma hiyo,” Tinsley aliongeza. ‘What3words‘ imeainisha namna ya kutambua kila eneo kwa namna yake.

 

Wavumbuzi wa programu hiyo ndiyo waliigawa dunia katika pande trilioni 57 kwa mita 3 na kila upande kuna maneno matatu ambayo hayana mpangilio kuainisha anuani ya sehemu husika.

Programu hii ilianza kutumiwa na muasisi wa kampuni hiyo, Chris Sheldrick, ambaye alipata changamoto hizo kwa kuwa alikuwa anaishi katika maeneo ya vijijini huko Hertfordshire, Uingereza.

 

“Tulikuwa tunapata barua za watu wengine katika nyumba yetu kwa sababu nyumba yetu ilikuwa haina anuani.” alisema.

Miaka kumi akiwa tasnia ya muziki ambayo alipata changamoto kubwa ya kuwasiliana na bendi mbalimbali kufika katika ukumbi, ilimlazimu kutafuta suluhu la tatizo linalomkabili.

 

“Nilijaribu njia mbalimbali za kufika eneo niliko bila mafanikio, hivyo ikanifanya niwaze zaidi njia ambayo ni rafiki”, Sheldrick alieleza.

Kampuni ya programu tumishi hiyo ilianza mwaka 2013 na sasa imewaajiri watu zaidi ya 10o kaskazini mwa mji wa London.

 

Gari aina ya Mercedes Benz imejumuisha programu hiyo katika mitambo yake ya gari na sasa what3words inatumika katika lugha 35.

“Kama watu hawana programu tumishi hiyo, huduma ya dharura inaweza kutuma ujumbe mfupi unaojumuisha anuani ya tovuti hiyo katika simu zao.

 

“Lakini programu-tumishi inahitaji mtandao wa Intanet ingawa haihitaji mtu kuwa na mtandao wa simu kusema maneno hayo matatu ya kujulisha eneo la mtu alipo,” Sheldrick alisema.

 

“Hata kama hamna mtandao eeo alipo bado mtu anaweza kusaidiwa kama atajua maneno matatu ya eneo husika.” alisisitiza.

Watu waliookolewa kupitia progamu hiyo wanawafanya waasisi wa programu hiyo kuwa wamefanya kazi ya maana kwa jamii.

Comments are closed.