The House of Favourite Newspapers

Machozi: Diamond ana ukubali mziki wangu

0

11887107_489827214528874_218821705_nMsanii wa kizazi kipya, Hussein Machozi.

LICHA ya kuonekana kama anapotea, msanii wa kizazi kipya, Hussein Machozi, amefunguka kuwa yeye bado yupo na anapiga mziki kama kawa na msanii anayetamba kimataifa zaidi Nasibu Abdul ‘Diamond’ amekuwa akisikiliza kazi zake.

Machozi ni mmoja kati ya wasanii walioweza kutamba kipindi cha nyuma kidogo kutokana na uwezo wake katika kazi kadhaa ambazo aliwahi kutoa kama Full Shangwe, Utaipenda, Kafia Gheto, Jela na nyingine kibao.

Akizungumza na Mikito Jumatano, Machozi alifunguka kuwa yeye bado yupo vizuri na hata msanii mwenzake Diamond licha ya kufanya vizuri pia anakubali kazi zake na bado hajafunikwa tatizo tu hajapata nafasi.

“Nafahamu nina kipaji cha kuimba hilo hata Daimond analitambua na kazi zangu anazikubali bila ubishi kwamba mimi najua nina uwezo hata wa kumfunika na ananifuatilia vizuri.

“Sisi wa zamani bado tupo juu sana wewe sema mziki wa sasa umetawaliwa na watu fulani fulani ndiyo maana tumekuwa tunashindwa kuchomoka. Sasa nimerejea Bongo nikitokea Kenya kwa ajili ya kupiga kazi,” alisema Machozi.

Leave A Reply