The House of Favourite Newspapers

Majambazi Yaua Polisi 4 Mbagala, Dar

0

MAUAJI YA POLISI

Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, Mbagala wilayani Temeke, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba  akimjulia hali Raia aliyejeruhiwa
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekamatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.
Waziri Nchemba na Kamanda Sirro wakiwa eneo la tukio

Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.

Gari ya Polisi ikiwa imezagaa Risasi

Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.

Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.

Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.

Polisi waliouawa ni pamoja na;

E5761 CPL YAHAYA

F4660 CPL HATIBU

G9544 PC TTITO.

Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 usiku katika na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.

Mmoja kati ya polisi waliouawa alikuwa anaingia lindo, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva na imeelezwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki ila gari la polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa  kwa risasi.

Leave A Reply