The House of Favourite Newspapers

Picha Kutoka Eneo la Tukio: Polisi Yakabiliana na Majambazi, Mkuranga

2

bunduki

Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.   mkuranga (4)Wananchi wa Mkuranga wakishudia tukio hilo.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru  zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

Aidha taarifa za awali ziliripoti kuwepo na majibizano ya risasi kati ya jeshi la Polisi na watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo ya Vikindu, mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo na inadaiwa kuwa askari mmoja ameuawa kwenye mapigano hayo.

mkuranga (2)Wananchi wakitaharuki

Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano hayo  kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.

Milio ya risasi na mabomu bado vinaendelea kusikika kunzia saa saba usiku wa kuamkia leo katika eneo hilo ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.

mkuranga (3)Mwandishi wa Global Publishers aliyeko eneo la tukio amesema kuwa mpaka sasa magari ya polisi yanaonekana yakiingia na kutoka katika eneo la tukio Vikindu kwenye nyumba walimojificha majambazi hao huku wananchi wakikusanyika kwa mbali kushuhudia tukio hilo la aina yake.

mkuranga (1)Kutoka eneo la tukio:

Hatimaye milio ya risasi haisikiki tena eneo la tukio ambapo polisi wanapambana na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi tangu usiku wa kuamkia leo, Mkuranga, Pwani.

Wanachi wameambiwa wasisogelee eneo la tukio.

Updates

Jeshi la Polisi limeweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, Mkuranga, magari yote yanayotoka na kuingia Dar yanapekuliwa kabla ya kuendelea na safari zake.

2 Comments
  1. samuel gulle says

    Ulinzi uimarishwe

  2. haji juma says

    Safi sana jeshi la polisi kwakuongeza nguvu eneo la tukio vikundi mko wengi mtashinda UJAMBAZI hongera SIRO raia wanyonge tunakutegemea COMANDA

Leave A Reply