The House of Favourite Newspapers

Majonzi Tupu Kuangwa Dada wa Bilionea Msuya

1

9.Waombolezaji wakipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu Anathe Msuya

1314.Dada wa marehemu akishindwa kujizuia na kulia kwa uchungu.158.Dada wa marehemu wakiuangalia mwili wa mpendwa wao.Dada wa marehemu wakiaga mwili wa ndugu yao.

101112716.Mtoto wa marehemu, Anathe aitwai Alan Kimario (aliyeko katikati akilala) akiwa kanisani hapo.

M toto wa marehemu Anathe, Allan Kimario (aliyelala).

2 3 4

15 14.Dada wa marehemu akishindwa kujizuia na kulia kwa uchungu. 13

Majonzi na huzuni vimetawala kwenye tukio la kuagwa kwa mwili wa mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa risasi mwaka 2013, Anathe  Simon Msuya ambaye yeye aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar, Mei 25 mwaka huu.

Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za mwisho.

Mtoto wa Anathe aliyetajwa kwa jina la Alan Kimario (4) alionekana akilazimishwa kwenda kuuaga mwili wa mama yake kwani alikuwa akitaka aachwe aendelee na michezo yake kutokana na ukweli kwamba, alikuwa hajui hata kinachoendelea.

Mwili wa marehemu Anathe umesafirishwa kwenda Mererani jijini Arusha kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho (Jumanne).

 Mungu ailaze roho ya marehemu Anathe mahali pema peponi. Amin!

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

1 Comment
  1. LEO says

    Mungu amlaze maala pema peponi maombi yafanyike kwa ajii ya familia nzima na mototo wa Marehem Amen

Leave A Reply