The House of Favourite Newspapers

Malinzi, Mwesigwa Wahukumiwa Jela, Warejea Uraiani

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo Jumatano Desemba 11, 2019 imemtia hatiani aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo huku aliyekuwa katibu wa shirikisho hilo, Slestine Mwesigwa akitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo.

 

 

Mahakama hiyo imewahukumu Jamal Malinzi na Selestine Mwesigwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya jumla ya Sh Milioni 1.5 ambapo wamekubali kulipa faini.

 

Kosa la kwanza washtakiwa wote wawili wamepigwa faini faini ya Tsh 500,000 kila mmoja au jela miaka miwili, na kosa la pili linalomkabili Mwesigwa peke yake amepigwa faini ya Tsh 500,000 au jela miaka miwili.

 

Aidha, Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya.

 

 

Katika shtaka hilo Malinzi alikuwa akidaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edagar Masoud aliwekwa Mwanga.

 

 

Katika kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.

TAZAMA VIDEO

Leave A Reply