The House of Favourite Newspapers

Maneno ya Magufuli yawakuna mastaa

0

egSalma Jabu ‘Nisha’.

Stori: Waandishi Wetu, wikienda
Dar es Salaam: Kwa nini Mungu hakumleta Magufuli mapema? Ndiyo kauli ya wikiendi iliyopita kufuatia maneno ya hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ wiki iliyopita juu ya kusafisha wizara, idara na taasisi za serikali kufuatia kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi.

Baada ya hotuba hiyo ambayo Rais Magufuli aliitoa Siku ya Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Mahakama (Siku ya Sheria), watu mbalimbali kutoka kila kona ndani na nje ya Bongo walionesha kuguswa nayo huku wakijenga imani kubwa kwa serikali yake.

Baadhi ya mastaa wa Kibongo waliozungumza na Ijumaa Wikienda walionesha kukunwa na maneno ya hotuba hiyo huku wakihoji kuwa kwa nini Wabongo hawakumpa nafasi hiyo mapema kwani nchi ingekuwa mbali kimaendeleo.

dude2Kulwa Kikumba ‘Dude’.

JACOB STEVEN ‘JB’:
“Magufuli ndiye kiboko ya mafisadi. Kiukweli amefufua matumaini ya Watanzania wengi waliokuwa wamekata tamaa ya maisha. Cha msingi ni kumuombea Mungu ili ampe ulinzi afanye kazi yake kisawasawa bila kutishwa.”

SALMA JABU ‘NISHA’:
“Maneno ya Magufuli yamekonga moyo wangu maana Watanzania walikuwa wakiibiwa lakini hawakuwa na mtetezi. Mimi namuomba aendelee kusafisha rushwa serikalini.”

BABY JOSEPH MADAHA:
“Jamani Magufuli alikuwa wapi mbona hakuja mapema? Yaani kweli amewakuna wengi kwa kuahidi kuwafunga mafisadi.”

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’:
“Huyo ndiye Magufuli lazima mafisadi watanyooka. Asafishe kila uchafu tuwajue na tuone wakifungwa jela.”

MAHSEIN AWADH ‘DK. CHENI’:
“Kiukweli ile hotuba ilikuwa kiboko na naamini haishii kwenye maneno tu kwani ninavyomjua anamaanisha. Anaonekana ana uchungu na maisha magumu ya Watanzania sasa roho inamuuma kuna watu wachache wanafaidi matunda wakati wengine wanateseka.”

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’:
“Ebwana ile hotuba ilikuwa maneno yenye matumaini mapya kwa Watanzania. Yaani watu walikuwa wanatamani aendelee kumwaga maneno kuntu.”

MRISHO MPOTO:
“Kiukweli Magufuli ndiye kiboko ya mafisadi. Kinachotakiwa ni kumuunga mkono maana anasema ukweli, mtu anakamatwa na vithibitisho halafu anangoja upelelezi, upelelezi wa nini?”

Leave A Reply