The House of Favourite Newspapers

Maonyesho ya Kwanza Bidhaa za Viwanda Nchini Yaanza Dar

MAONYESHO ya bidhaa za viwanda zinazozalishwa hapa nchini yameanza leo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Barabara ya Kilwa. 2       

Kamera yetu ilifika kwenye maonyesho hayo na kujionea shughuli mbalimbali za biashara zikiendelea ambapo pia miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni banda la mchele ulio katika viroba, chumvi kutoka Bagamoyo na korosho kutoka Mtwara.

1Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Edwin Rutageruka, akiangalia bidhaa za Mshauri na Mtafiti wa Masuala ya Afya, Ester Mtwalizya, kutoka kampuni ya Ideal Heath Care.

Maonyesho hayo ambayo yameanza katika viwanja vya Saba Saba, yatazinduliwa kesho rasmi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, yanategemewa kuendelea hadi Desemba 11 mwaka huu.

3Meneja Biashara wa Maendeleo wa kampuni inayozalisha chumvi iitwayo Seasalt ya Bagamoyo, Pwani, Deodatus Timothy, akizungumza na Global TV Online.

4Baadhi ya wananchi wakitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini.

5Mwanamama aitwaye, Fatuma Ulenje (kulia) akiwa na wananchi waliofika katika banda lake linalouza korosho zinazozalishwa katika kiwanda cha Tandahimba, mkoani Mtwara.

6Banda la muuzaji wa mchele, Kenam Sanga (kulia) wa Usangu Marketing Co Ltd.

7Raia wa China wakiwa katika banda la mwanamama, Fatuma Ulenje lenye kuzalisha korosho.

9Muuzaji wa vifaa vya ujenzi, Baseke Richard, akiwa katika banda lake.

8Baadhi ya mabango ya bidhaa zilizopo kwenye maonyesho hayo.

10Bidhaa za mchele zikiwa katika maonyesho hayo.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.