The House of Favourite Newspapers

Masanja aibuka na oparesheni ya mtaani

0

Maono! ‘Hapa Kazi Tu’ inazidi kushika kasi baada ya Mwimbaji, Mchekeshaji na Mchungaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ kuamua kuibuka na oparesheni ya kuhubiri Injili mitaani.

Akizungumza na Over Ze Weekend, alisema alichoamua ni kufanya oparesheni ya kuhubiri Injili mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.

“Mwanawane hii ni oparesheni ya mitaa yote ya Dar ili watu wamrudie Mungu, nikiwa na wainjilisti kutoka Mito ya Baraka tumeweza kuhubiri maeneo ya Kariakoo, Karume, Tabata Segerea ,Tabata Kimanga, Mbagala pamoja na Kibamba,” alisema Masanja.

Leave A Reply