The House of Favourite Newspapers

Masau Bwire akataa simu ya Haji Manara

OFISA Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa hawezi kuchukua simu aliyopewa na msemaji wa Simba, Haji Manara, kwa kuwa hapendi kutumia ‘masimu’ makubwa.

 

Hatua hiyo imekuja, ikiwa imepita siku chache tangu Manara aandike kwenye mtandao wake wa Instagram kuwa, atamkabidhi simu mpya aina ya iphone eleven Masau ili aache kutembea na simu nyingi za bukubuku. Masau amekuwa na kawaida ya kutembea na simu nyingi kila anapokuwa.

 

Sasa baada ya Simba kushinda juzi kwa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu, Manara aliweka video kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa ameshika simu mbili aina ya iphone na kusema: “Masau chagua hapa unataka ipi, kuna iphone eleven na iphone 10, chagua nikuletee wapi, shule au kambini ili uache kutumiatumia makopo.”

 

Kufuatia kauli hiyo, Masau alisema: “Mimi sipendi kuzungumzia maisha zaidi, kwa sababu Watanzania wanafikiri ukiwa na simu kubwa ndiyo una maisha mazuri, mimi siipendi iphone hata ukiniletea hapa naipasua, mimi simu zangu naagiza Marekani, unapata vitu ambavyo hata kwenye simu nyingine haupati.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Comments are closed.