The House of Favourite Newspapers

Massauni: Ajali Barabarani Zimepungua kwa Asilimia 10

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani mhandisi Hamad Massauni ameeleza mafanikio ambayo yamefanywa na baraza hilo na kufanikiwa  kupunguza vifo na majeruhi wa ajali za barabarani kwa asilimia 10 ambapo katika kipindi cha miezi sita, vifo vimepungua kwa asilimia 19.

1-001

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Mhandisi Hamad Massauni akisoma taarifa kwa wanahabari (hawapo pichani).

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na wanahabari  na kutoa  tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa baraza hilo katika kupunguza ajali za barabani.

Aidha alisema kuwa miongoni mwa malengo makubwa ya tathmini hiyo ni kupunguza ajali, vifo na majeruhi, ukamataji wa makosa ya usalama barabarani  kwa magari na pikipiki, elimu ya usalama barabani kwa watumiaji wa barabara na hata usimamizi wa sheria.

2-001

…Akionyesha msisitizo wa jambo kwa wanahabari.

Alifafanua kuwa tathmini ilionyesha kuwa miezi miwili kabla ya mkakati huo makosa mbalimbali ya usalama barabarani yalikuwa ni 324,284 katika miezi miwili na  baada ya mkakati kulikuwa na  makosa 393,728 ambalo ni  ongezeko la makosa 69,444  ambayo ni sawa na asilimia 21.

3-001

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

Alieleza pia kipindi hicho cha miezi miwili kabla ya mkakati kulikuwa majeruhi 135 na miezi miwili baada ya mkakati kulikuwa na  majeruhi 113 na kuonyesha upungufu wa majeruhi 22 ambayo ni sawa na asilimia 16.

Vilevile amewataka wajumbe wa baraza hilo kushiriki katika kufanya oparesheni katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na kamati za usalama barabarani za mikoa na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa mkakati huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo.

Na Denis Mtima/Gpl

Comments are closed.