The House of Favourite Newspapers

Matatizo Katika Shingo Ya Kizazi

0

ovariancystdiagram.jpgTatizo hili linaweza kuwa la kuzaliwa nalo, likasababishwa na matumizi ya baadhi ya madawa kwa mama mjamzito ukajikuta unazaa mtoto anapata kasoro katika viungo vyake mojawapo ni viungo vya uzazi.

Tatizo katika viungo vya uzazi pia linaweza kusababishwa na maambukizi, upasuaji au magonjwa sugu katika uke au shingo ya uzazi.

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu wakati wa tendo la kujamiana au kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo. Vile vile kutokwa na uchafu ukeni unaotoa harufu au muwasho, ingawa wakati mwingine anaweza kupata ute mzito daima.

VIGEZO VYA UCHUNGUZI

Katika suala zima la ugumba kwa mwanaume na mwanamke lazima kuwepo na vigezo vya uchunguzi. Kwa mwanamke mambo ya kuangalia ni historia yake katika matumizi ya madawa ya tiba alipokuwa mdogo au hata kama mama yake aliwahi kutumia aina fulani za madawa wakati wa ujauzito.

Tutaangalia kama ulivunja ungo kwa wakati muafaka, mfano uliwahi sana au ulichelewa sana. Muda muafaka ni kati ya miaka 12 hadi 16. Kufahamu mzunguko wako wa hedhi unavyoenda na kiwango cha damu unachopata, kama ulishawahi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango, je, ulishawahi kupata mimba? Na ulizaa au iliharibika?

Vilevile inahitajika kujua kama ulishawahi kufanyiwa upasuaji wowote chini ya tumbo mfano kutoa uvimbe, mimba nje ya kizazi, kuzaa mtoto kwa upasuaji. Ni muhimu pia daktari akafahamu endapo ulishawahi kupata maambukizi yoyote katika viungo vya uzazi, madawa uliyokwishawahi kutumia kwa muda mrefu, ulaji wako wa vyakula, kama unakunywa pombe au unavuta sigara.

Kwa upande wa mwanamke, vigezo ni kama una kasoro katika viungo vyako vya uzazi, mfano uume ni mfupi sana, tundu la mkojo limekaa upande, kasoro katika korodani au kende kama zipo, zimevimba, zimesinyaa au ndogo sana, hazipo au ipo moja, zinauma au moja ndogo na nyingine kubwa.

Pia utahitajika kujua kama ulishawahi kusumbuliwa na maambukizi katika njia ya mkojo kwa muda mrefu, mfano kisonono au yutiai za mara kwa mara, maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa na majimaji au manii katika njia ya mkojo.

Inahitajika kujua historia yako kama ulishawahi kumpa mimba mwanamke, kama una mtoto. Ufanyaji wako wa tendo la kujamiiana pia daktari itabidi ajue endapo huwezi kabisa, kumudu, unawahi kumaliza, unachoka sana baada ya tendo au unashindwa kurudia, au uume hauna nguvu za kutosha.

Ni muhimu kuelezea kama unakunywa pombe, unavuta sigara au unatumia madawa ya kulevya kama bangi, mirungi na mengineyo. Vyote hivi huathiri uzazi kwa kiasi kikubwa. Je, ulishawahi kufanyiwa upasuaji hasa wa henia au ngiri ya kushuka, busha, vyote inabidi vijulikane.

Matumizi ya madawa ya kulevya ya hospitali kwa muda mrefu, mfano dawa kwa ajili ya vidonda vya tumbo, kifafa, moyo, kifua kikuu na mengineyo. Ulaji wako wa chakula na ufanyaji mazoezi, vilevile kuangalia unanyoa sehemu za siri na makwapani baada ya muda gani, kwani nayo huchangia kuashiria baadhi ya dalili.

Kwa hiyo, ukiangalia kwa undani kuhusiana na suala zima la kutopata mtoto, siyo tu kwamba mtu anatumia dawa fulani na kufanikiwa.

Pia suala hili halitibiwi kwa hisia na utabiri, bali ni suala la kisayansi na linahitaji uchunguzi wa kina na tiba za hospitali.

Vyanzo vya matatizo haya ni vingi na tofauti ni kubwa inayomtokea kila mwenye tatizo. Tumeona vigezo.

NINI CHA KUFANYA?

Katika makala ijayo tutaona kwa undani kuhusiana na vipimo vya msingi, tiba na ushauri ili usije ukapata tatizo au kama ulikuwa nalo likatibika, basi lisijirudie.

Tatizo hili la kutokupata mtoto au ugumba kama tulivyokwishaona hapo awali, linawahusu mke na mume na hakuna sehemu watakayopata tiba sahihi zaidi ya hospitali za mikoa ambako kuna madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi.

Leave A Reply