The House of Favourite Newspapers

Matatizo ya kutoona vizuri

0

Baada ya wiki iliyopita kufikia tamati kwa makala iliyohusiana na mzio (Allegy), leo nawaletea mada inayohusu matatizo ya macho ambayo yamekuwa yakiwakumba watu wazima na watoto. Ungana nami…

Uoni hafifu wa macho ni hali ya kupoteza ukali wa macho kuona  jambo linalofanya vitu visionekane au vififie machoni.

Sababu kuu za kufifia kwa uono wa macho ni hitilafu zinazobadili mwelekeo wa nuru ya macho Refractive errors.
Wengine huwa na uoni wa karibu Shortsightedness na kushindwa kuona mbali, wengine huona mbali na kuona kwa shida vitu vikiwa karibu yao Farsightedness na wengine huwa na shida ya kuona vizuri hata vitu vilivyo karibu Astigmatism, tatizo hili pia linaitwa Presbyopia, mara nyingi, hujitokeza kwa wazee wenye umri mkubwa zaidi.

Lakini kufifia kwa nuru ya macho pia kwaweza kuwa dalili ya matatizo mengine ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayohatarisha uoni wa macho na matatizo ya mishipa ya ubongo. Tatizo la kufifia kwa uoni laweza kuathiri macho yote lakini baadhi ya watu hupata tatizo hili katika jicho moja tu.

Lakini uonaji wa mawingumawingu au mawimbimawimbi ni dalili ya matatizo jichoni kama vile mtoto wa jicho Cataract au huweza kuwa dalili ya tatizo kubwa la macho.

Daktari wa macho anaweza kupima kiwango cha kufifia kwa nuru ya macho yako na kubaini sababu kwa kukufanyia uchunguzi kamili ikiwa ni pamoja na vipimo vya Spatial Contrast Sensitivity, Slit-lamp na Standard Snellen hivyo ukiona dalili hizo muone daktari haraka.

Wiki ijayo; sababu na matibabu ya uoni hafifu wa macho, usikose nakala yako.

Leave A Reply