The House of Favourite Newspapers

Mawigi: Namzimia Niyonzima Hadi Naumwa

mary-mawigi
Dar es Salaam: Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Mary Mawigi (pichani juu) ameibuka na kudai kuwa, anamzimia mwanakabumbu Haruna Niyonzima wa Yanga ambapo kuna wakati akienda uwanjani, hujikuta akiumwa.

Akipiga stori na Wikienda, Mawigi alisema licha ya yeye kuwa shabiki wa kutupwa wa Yanga lakini huwa akienda uwanjani, akimkosa mcheza huyo hujikuta anapatwa na homa kwani anampenda kupita kiasi.

NIYONZIMANEW4

Haruna Niyonzima.

Wikienda lilipomhoji sababu za kumpenda mume wa mtu kiasi hicho, Mawigi alidai kuwa hajali kama ni mume wa mtu au ana familia kwa kuwa anampenda tu kama shabiki wake na hakuna anayeweza kulizuia hilo.

“Hakuna anayeweza kunizuia kwani naelezea kilicho moyoni mwangu,” alisema Mawigi.

Stori: Hamida Hassan, Wikienda

Comments are closed.