The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kusimamisha Msafara wa Rais na Kuomba Kazi

0

MWANAMME mmoja aliyejulikana kwa jina la Uvinalies Nyabuto amekamatwa leo kwa kuusimamisha msafara wa magari wa Rais Uhuru Kenyatta katika barabara ya kuelekea Ikulu.

 

Kwa mujibu wa Polisi, msafara huo ulikuwa unaelekea Ikulu ukitokea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) ambapo Rais Kenyatta alitoka kwenye mkutano wa 9 wa Wakuu wa Nchi za Caribbean na Pacific.

 

Nyabuto alisimamisha msafara akiwa ameshika bango lililoandikwa “Mheshimiwa, Tafadhali naomba nafasi ya kujiunga na Majeshi ya Ulinzi. Nisamehe kwa kutoheshimu Ulinzi wako. Samahani Rais. Nyabuto.”.

 

Mara moja alikamatwa na Walinzi walio kwenye msafara wa Rais na baadaye alipelekwa katika Kituo cha Polisi Kilimani ambapo aliendelea kushikiliwa.

 

Leave A Reply