The House of Favourite Newspapers

Mbongo atekwa, ateswa ughaibuni!

0

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (1) Mtanzania Adam Akida Mwinyimkuu akiwa ametekwa.

Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI

DAR ES SALAAM: Mtanzania Adam Akida Mwinyimkuu, mkazi wa Magomeni jijini hapa, ametekwa ughaibuni na watu wanaoaminika kuwa ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ‘Wazungu wa Unga’ ambapo kisa kinaonekana kuwa ni Mbongo huyo kuwekwa dhamana au ‘gerenta’ (bond) na wauza unga wa hapa nchini, Uwazi limechimba.

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (6)…Akipata mateso na kupigwa.

NDUGU WA ADAM WANAJUA

Taarifa za Adam kutekwa ziliwafikia ndugu zake, wakiwemo wazazi wake wanaoishi Mapinga wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambao walihamia huko mwishoni mwa mwaka jana baada ya nyumba yao ya mabondeni, Magomeni kubomolewa.

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (5)VIDEO YATUPWA MTANDAONI

Video inayomwonesha Adam akiwa chini ya udhibiti wa mitutu miwili ya bunduki, ilitupiwa kwenye mtandao na watu hao wakimshurutisha kusema kwao ni wapi na nani aliyemtuma.

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (4)ANACHOKISEMA MBELE YA MITUTU

Adam ili kuokoa maisha yake, anaonekana akisema yote kwamba, anaitwa Adam Akida Mwinyimkuu, mkazi wa Magomeni jijini hapa. Lakini pia anamtaja mtu mmoja kwa jina la Juma, mkazi wa Kunduchi, Dar kwamba ndiye aliyemweka dhamana huko ughaibuni na kuomba msaada kutoka kwa nduguze.

“Mwambieni Juma alete hela za watu, mimi nimewekwa geleka huku. Nyumbani kwetu ni Magomeni, Mtaa wa Chemchemi na Idrisa, baba yangu anaitwa Akida, mama Rukia Daudi,” anasikika akisema Adam kwenye video hiyo.

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (3)MATESO MAKUBWA

Hata hivyo, akiwa bado anaendelea kujieleza, watu hao waliofunika sura zao wakiwa wamevalia kanzu na suruali pana mfano wa pajama zenye rangi ya kijivu, wanaonekana wakimshika Adam na kumsulubu, kitendo kinachomfanya Mbongo huyo kupiga kelele akiomba asiuawe kwa vile midomo ya bunduki imemwelekea.

MBONGO ATESWA-PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (2)UWAZI KATIKA KUCHIMBA

Ili kuipata habari hiyo kwa kina, Uwazi lilifuatilia maelekezo ya Adam kwa kwenda Magomeni na kukutana na watu ambao walikiri kumfahamu baada ya kuoneshwa video hiyo.

“Aah! Huyu ni Adam. Alikuwa akifanya kazi ya kunyoa kwenye saluni, nendeni kwenye nyumba ile pale yenye mti nje, mkiwauliza pale lazima watawaambia kila kitu na kuwapeleka mpaka nyumbani kwao.

ughaibuni (1) Saluni aliyokuwa akifanya kazi Adam nyumbani kwao Magomeni.

“Huyu jamaa alikuwa kinyozi pale, alipoondoka alisema anakwenda Pakistan lakini hakusema anafuata nini,” alisema mtu mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.

Makachero wetu walifika kwenye saluni hiyo ambayo kwa sasa imefungwa na kumkuta dada aliyejitambulisha kwa jina la Mwajuma.

ughaibuni (2)Mama mdogo wa Adam

Akizungumza na gazeti hili baada ya kuoneshwa video hiyo, Mwajuma alisema: “Dah! Jamani kweli inasikitisha, yaani Adam huyuhuyu ndiyo anateswa hivi!

“Alikuwa akinyoa kwenye hii saluni mnayoiona lakini tangu apotee hapa mtaani karibu mwaka mmoja umepita, tulikuwa hatujui alipo. Lakini mkitaka kujua zaidi ni vizuri mfike nyumbani kwao ambapo si mbali na hapa.”

Baada ya kufika nyumbani hapo, makachero wetu walikaribishwa na Hadija Katundu ambaye alijitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Adam.

“Mimi ni mama’ke mdogo, niliyeolewa na baba yake mdogo Adam, aitwae Kessy Mwinyimkuu ambaye amezaliwa tumbo moja na baba yake mzazi, Akida Mwinyimkuu.

“Tayari taarifa hizo zimeshafika kwa familia na watu wako kwenye harakati za kushughulikia tatizo hilo ili kumkomboa kijana wetu.

“Kwa kweli inasikitisha sana masikini ya Mungu. Huyu kijana tangu aondoke huu sasa unakaribia mwaka na hatukuwa na taarifa zake zozote za kazi anayofanya huko aliko, ndiyo hivi karibuni tukapata taarifa za kutekwa kwake na hao maharamia.

“Wazazi wake wote wawili tulikuwa tukiishi nao kwenye nyumba hii lakini kwa sasa wamehamia Mapinga, Bagamoyo,” alisema mama mdogo huyo.

ADAM NA MKEWE

Mama huyo aliendelea kusema kuwa, Adam alipoondoka aliacha mke na watoto wawili ambao wanaishi Kijitonyama, Dar.

Uwazi lilimtafuta kwa njia ya simu baba mdogo wa Adam ambaye hakuwepo nyumbani hapo wakati mkewe akizungumza na gazeti hili lakini simu yake haikupokelewa kila ilipopigwa mpaka tunaelekea mitamboni.

Juzi, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya,  SACP Mihayo Msikhela ambaye alisema tayari video hiyo wanayo na kwamba, wameshaanza kuwasaka wanaotajwa ndani yake kwa ajili ya mahojiano.

“Tunayo hiyo video, wote waliotajwa tumeanza kuwahoji ili kuwasikia,” alisema kamanda huyo.

KUWEKWA BOND

Kuwekwa bond maana yake, mzungu wa unga anamchukua Mbongo kwenda naye ughaibuni, akifika kule anapewa unga kwenda kuuza kwa makubaliano ya kumwacha mtu huyo akiwa amesalimisha hati ya kusafiria na nyaraka nyingine muhimu. Akishauza unga, anarudisha pesa, anapewa mtu wake.

Inapotokea biashara haijawa nzuri, aliyepewa unga amekamatwa au ameuza na kukimbia na pesa, ndipo watoa unga humteka na kumtesa mtu huyo aliyewekwa bond na video yake kuirusha mtandaoni kwa lengo la kushinikiza kupewa pesa yao.

CHEKI PICHA AKITESWA

Leave A Reply