The House of Favourite Newspapers

Mchepuko atorosha mke wa mtu!

0

P1310011lsihaka Makulunga akionyesha hati ya ndoa.

Stori: DUSTAN SHEKIDELE, Wikienda

Morogoro: Wakati dunia ikielekea Siku ya Wapendao (Valentines Day) ambayo huadhimishwa Februari 14 ya kila mwaka, mfanyabiashara lsihaka Makulunga (33), mkazi wa mjini hapa anadai kutorokwa na mkewe, Mwajuma Mohamed (28) aliyetimkia jijini Dar kwa mchepuko ili kula bata za siku hiyo ya wapendanao.

Kwa mujibu wa Makulunga, alifunga ndoa ya Kiislam na Mwajuma mwaka 2013 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kike kabla ya kutoroshwa nyumbani na mchepuko mwishoni mwa wiki iliyopita.

Makulunga anayefanyia biashara zake kwenye soko kuu mjini hapa anadai kuchanganyikiwa kiasi cha kutembea barabarani na cheti cha ndoa na picha za mwanamke huyo huku akiomba msaada wa mawazo.
“Hapa nakwenda Bakwata kuvunja ndoa yangu. Mke wangu katoroshwa na mchepuko wake, kaenda Dar kwa bwana’ke aliyemwalika wakale Valentine’s Day,” alisema Makulunga kwa masikitiko makubwa na kuongeza:

P1310009Mwajuma Mohamed anayedaiwa kumtoroka mumewe.

“Hivi karibuni mke wangu alibadilika kitabia, akawa anachati na mwanaume, nilikuta meseji zaidi ya kumi za kimapenzi nilipofuatilia niligundua mke wangu ana mchepuko tena upo Dar umemwalika Valentine’s Day na kweli ametorokea huko.

Alipotafutwa mwanaume anayedaiwa kumtorosha Mwajuma na kusomewa mashtaka yake alijitetea kuwa yupo kwenye daladala hivyo akishuka atapiga simu kwa mwandishi wetu lakini hakufanya hivyo na hata alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa kisha ikazimwa.

Leave A Reply