The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Asakwa kwa Kuwapa Mimba Wanafunzi 20

0

MAOFISA Usalama wa Kaunti ya Kitui nchini Kenya, wanamsaka mhubiri mmoja (jina halikutajwa) anayedaiwa kuwahadaa na kuwapa ujauzito wasichana wadogo takriban wanafunzi 20.

 

Inaarifiwa kuwa mhubiri huyo amekuwa akiwabaka wasichana hao kwa nyakati tofauti na kwamba amekuwa akiwakaribisha nyumbani kwake kwa kuwaahidi kuwaombea ili wafaulu mtihani wao wa Darasa la Nane.

 

Imedaiwa kwamba, kutokana na uhitaji wa ufaulu, wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mchungaji huyo na kisha baadaye kujikuta katika manyanyaso ya kingono.

 

Katika kisa cha mchungaji huyo mwenye tamaa ya kuwatenda vibaya kondoo wake, baadhi ya wakazi wa Kasunti walimgutukia na kuanza kumfuatilia.

 

Duru kwenye eneo hilo ziliarifu kuwa, mtumishi huyo wa Bwana amekuwa akitumia vileo fulani kuwamaliza nguvu watoto hao kabla ya kuwafanyia unyama huo.

 

Kamanda wa Polisi Kituo cha Mwingi Kaskazini, Peter Mutuma alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa tayari wasichana kumi waliokolewa kutoka kwenye nyumba moja walipokuwa wamefichwa na mchungaji huyo.

 

Inaelezwa kuwa Alhamisi Novemba 28 mwaka huu, mzazi mmoja alimfungia kazi mchungaji huyo baada ya kupata habari kuwa msichana wake alikuwa akitumikishwa kingono.

 

Kwa ujasiri mama huyo alivamia nyumbani kwa mchungaji akiwa na hamaki na ndipo maovu mengine mengi yakafichuka. Duru za kipolisi zimearifu kuwa mchungaji huyo alifanikiwa kuwatoroka polisi ambao baadaye walimkamata mkewe kwa lengo la kuwasaidia uchunguzi wakati wakimsaka mumewe.

Leave A Reply