The House of Favourite Newspapers

Mdahalo wa Marekani: Trump Aonesha Chuki Dhidi ya Clinton

donald-trump-hillary-clinton-zoom-e55a3b65-f1ef-4ea3-a590-8586f4a4ada1Donald Trump na Hillary Clinton.

WAGOMBEA urais nchini Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump, walikutana tena katika mdahalo mkali usiku wa kuamkia leo ambapo pamoja na kutosalimiana kwa kupeana mikono, ambapo pia Trump wa chama cha Republican alitumia mdahalo huo kujitetea kuhusu maneno makali aliyoyatoa dhidi ya wanawake ikiwa ni dalili ya wazi ya kumshambulia Clinton wa chama cha Democratic.

Katika mpambano huo ambapo utamfanya mmoja wao kuwa rais wa 45 wa Marekani, Trump alikana kuwanyanyasa wanawake kingono na akageuzia hasira zake kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Bill Clinton mume wa mgombea mwenzake.

 “Hakuna mtu katika historia ya siasa ambaye amewanyanyasa wanawake kiasi hicho kana (Bill) Clinton,” alisema.

Matamshi ya Trump dhidi ya familia ya Clinton yalijiri baada ya mwendesha mjadala, Anderson Cooper,  kumuuliza kuhusu kanda ya video ya mwaka 2005 iliyosambazwa katika vyombo vya habari Ijumaa iliyomfichua Trump akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu zao za siri.

Alipoendelea kuulizwa kuhusu iwapo alimnyanyasa kingono mwanamke yeyote, alikana kufanya hivyo na badala yake akaongelea tuhuma zilizomuandama Bill Clinton katika siku za nyuma.

Hakuna mashtaka ya uhalifu yaliyowasilishwa dhidi ya Clinton katika tuhuma zozote za unyanyasaji wa kingono.

Wagombea hao wawili pia walizozana kuhusu mzozo wa Syria, uchokozi wa Urusi, na hatua ya Trump kukataa kutangaza malipo yake ya kodi na mpango wake wa kuwafanyia ukaguzi mkali  wahamiaji wanaowasili Marekani kutoka mataifa yanayohusishwa na ugaidi.

Mjadala huo ulikamilika wakati mwanaume mmoja miongoni mwa wasikilizaji alipowauliza wagombea hao wawili kila mmoja kusema kitu kimoja kizuri kuhusu mwenzake ambapo Clinton alisema watoto wa Trump wanamdhihirisha ni mtu wa aina gani, ambapo Trump alimtaja mpinzani wake kuwa “mpiganaji” asiyekata tamaa.

 

 

Comments are closed.