Meek Mill Ahukumiwa Kifungo Tena
Meek Mill
RAPA maarufu duniani anayetoka jimbo la Philadelphia nchini Marekani, Meek Mill ameamuliwa kutumikia tena kifungo cha miezi mitatu nje ya jera, baada ya kukiuka masharti ya kifungo chake cha awali ambacho hakutakiwa kutoka nje ya jimbo hilo wala kufanya shoo yeyote nje na Marekani jambo ambalo yeye alikiuka mwezi Desemba.
#BREAKING: Philly rapper Meek Mill sentenced to three months of house arrest. https://t.co/7mxixi4rR4pic.twitter.com/NTqDLwk1iu
— FOX 29 (@FOX29philly) February 5, 2016
Hukumu hiyo imetolewa jana Februari 2, na Jaji Genece Brinkley aliyekuwa akiendesha kesi yake.
Taarifa kutoka jarida la TMZ, rapa huyo mwenye umri wa miaka 28, ameamuliwa na mahakama kutumikia kifungo hicho kwa siku zisizopungua 90, huku akitakiwa kutorapu, kufanya shoo ya aina yeyote, au kutoa wimbo mpya kwa kipindi chote cha kifungo chake hicho.
FOX 29 imeripoti kuwa, Meek amepewa muda wa miaka sita kama muda wa matazamio kutokana na tabia zake chafu, endapo hatabadilika mwenendo wake basi mahakama itamchukulia hatua nyingine za kisheria.
Meek amekuwa kwenye muda wa matazamio tangu mwaka 2009 kuhusiana na skendo zake za madawa ya kulevya na matumizi mabaya ya silaha.