The House of Favourite Newspapers

Mgombea Morogoro Aangua Kilio Kisa Kushindwa

0

Aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Chamwino Adrew Boniface akilia.

Dustan Shekidele, Morogoro


Adrew Boniface aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Chamwino mkoani hapa kupitia Chadema na Mtangazaji wa Kituo cha Radio Planet, amejikuta akitokwa na machozi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

…Akiwa mwenye masikitiko.

Tukio hilo lilitokea juzi wakati mgombea huyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo kufuatia hujuma aliyofanyiwa na wakala wake kiasi cha kumfanya ashindwe katika dakika za mwisho.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye Viwanja vya Zahanati ya Chamwino huku machozi yakimbubujika, Andrew alidai kuwa mmoja wa mawakala wake alihongwa ili kumhujumu, kitendo ambacho kimemuumiza kwani anaamini alistahili kuibuka na ushindi mnono.

“Awali sisi viongozi tulipita katika vituo vyote na kujumlisha kura zilizobandikwa vituoni na kubaini tumeshinda kwa kura nyingi na wananchi wakaanza kushangilia huku wakishinikiza matokeo yatangazwe.“Hata hivyo, hayakutangazwa na baadaye mmoja wa mawakala wetu alituambia kwamba wakala wetu katika zoezi hilo la kuhesabu kura za jumla ametuhujumu na kukubali kwamba mgombea wa CCM ndiye mshindi, jambo ambalo wananchi wangu wamelipinga,” alidai mgombea huyo.

Kufuatia maelezo hayo, mgombea huyo aliwapa hasira wafuasi wake walioanza kufanya vurugu kupinga ushindi wa mgombea wa CCM, Benson Makanjira hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kufanikiwa kuwatuliza.

Leave A Reply