The House of Favourite Newspapers

Mgongano wa Kifikra Bongo Muvi ni Kaburi Jipya la Tasnia Hiyo

0

Na Ally Katalambula|IJUMAA WIKIENDA

Aprili 20, mwaka huu wasanii wa filamu za Kibongo nchini walifanya maandamo ya amani sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama lengo kubwa likiwa kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo huuzwa kwa bei chee na kuharibu soko la filamu zao.
Hata hivyo, katika mchakato huo kuliibuka  hoja na maswali lukuki kutoka kwa wadau wa filamu miongoni mwao wakiwa ni baadhi ya wasanii wenzao kutoka Bongo Muvi ambao  hawakukubaliana moja kwa moja na mchakato huo.
Hoja kubwa iliyoibuka ni kwamba siyo uuzwaji holela wa filamu za nje kwa bei chee ndiyo chanzo cha anguko la soko la muvi za Kibongo bali ni ubovu wa filamu za Kibongo.
Mgongano wa kifikra juu ya jambo hili miongoni mwa wasanii wa filamu ulizidi kupamba moto katika mitandao ya kijami huku hali hiyo ikitafsiriwa kama kaburi jingine jipya la kifo cha Bongo Muvi.
Tafsiri hii inatokana na ukweli kwamba kama wasanii wenyewe wanashindwa kuzungumza lugha inayofanana kubainisha na kutafuta ufumbuzi wa tatizo la anguko la soko lao ni wazi watakuwa wakicheza ‘marktime’ katika barabara ya kuwafikisha kwenye mafanikio.
Yafauatayo ni baadhi ya maoni ambayo Ijumaa Wikienda  lilifanikiwa kuyapata kutoka baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi lililofanyanao mahojiano kufuatia maandamano hayo.
Steve Nyerere
Wasanii wengi ni waoga, wanashindwa kuzungumza ukweli juu ya nini kinachofanya soko la filamu zetu kudorora, ukweli ni kwamba filamu zetu hazina ubora, tumeishiwa ubunifu ukilinganisha na tulivyoanza, mbona kipindi cha nyuma tulifanya vizuri ilihali hizo filamu za nyuma zilikuwepo tena ziliuzwa kwa bei rahisi kabisa. Kinachotakiwa ni kuzungumza ukweli kwa viongozi na tuone nini wanaweza kutusaidia ili tuendane na mahitaji ya Watanzania kwa sasa.
SIMONI  MWAKIFWAMBA
Mimi bado swali langu kwa hao waliofanya maandamo ni lilelile,  je tupige marufuku kuonyesha ligi za mpira wa miguu za nje kisa ya ligi kuu yetu ya ndani haifanyi vizuri? Jibu ni hapana kwa hiyo kuna namna ya kujipanga kwa mbinu zingine na siyo haya yanayofanyika kwa sasa.
DUMA
Filamu za nje ni vema zikomeshwe kabisa, ukweli ni kwamba hizi ni filamu nzuri na zina mvuto, utengenezaji wao ni wa kiwango cha juu kwakuwa wenzetu wamewekeza  vya kutosha, tofauti na sisi, hata hivyo filamu hizo zinauzwa kwa bei rahisi kwa wateja wetu. Unategemea nini zaidi ya kupotea kwa soko letu?

Leave A Reply