The House of Favourite Newspapers

Miaka 1,400: Hatimaye Wazungu Warudisha Ubao wa Yesu Bethlehem

0

  KIPANDE cha ubao kinachoaminiwa kuwa kilitolewa sehemu Yesu alipozaliwa kimerejeshwa mjini Bethlehem katika mji wa Jerusalem nchini Palestina baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,400.

Papa Francis aliagiza kurejeshwa kwa ubao huo uliokuwa Kanisa la Roma la Basilica ya Santa Maria Maggiore tangu karne ya saba.

Kibao hicho kilipokelewa mjini Bethlehem siku ya Jumapili na bendi ya gwaride na kuchukuliwa katika kanisa la Mt. Catherine, karibu na Kanisa la Nativity, Ukingo wa Magharibi ambako wataalamu wa masuala ya utamaduni wanasema Yesu alizaliwa hapo.

Kipande hicho cha ubao ni muhimu kwani baadhi ya Wakristo wanaamini ni sehemu ya mahali ambamo Yesu alilazwa baada ya kuzaliwa.

Tukio hilo linakwenda sambamba na kipindi cha Majilio, cha wiki nne kuelekea Krismasi.  Mji wa Bethlehem ambao unakaliwa na Israel katika Ukingo wa Magharibi unajitayarisha katika kushereheka tukio hilo ambapo mahujaji hufurika huko kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Idadi ya Wakristo katika Wapalestina ni ndogo, na Bethlehem ni moja ya miji michache katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza ambako Krismasi husherehekewa.

Leave A Reply