The House of Favourite Newspapers

Mike Tee aishauri Cosota

0

Mike-tee-mnyaluMkongwe wa Hip Hop-Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’.

Chande Abdallah, UWAZI

Mkongwe wa Hip Hop-Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’ amekishauri Chama cha Hatimiliki Tanzania (Cosota) kuzunguka mikoani na kutoa elimu kwa wasanii kabla ya kuingia kwenye mfumo wa malipo kupitia vyombo vya habari vinavyorusha kazi zao.

Akipiga stori katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni na Global TV Online, Mike Tee alisema kuwa, wasanii wengi wa Dar huwa na uelewa kwa kuwa huweza kuhudhuria vikao mbalimbali vya wasanii na wadau wa burudani kuliko wale wa mikoani.

“Wasanii hawana elimu ya mambo ya kulipwa kupitia nyimbo zao kupigwa redioni au kwenye runinga, wanatakiwa kwanza wafahamu madhara na faida yake hasa kwa wasanii chipukizi, hilo ni jukumu la Cosota kutoa elimu hiyo,” alisema Mike Tee.

Leave A Reply