The House of Favourite Newspapers

Mkuki Moyoni Mwangu – 36

0

ILIPOISHIA…

Catarina akidhani ameuchinja baada ya kupata safari kuelekea NewYork ambako aliahidiwa na Mario Pizaro kwamba angetafutiwa kampuni nyingine ya mitindo na kufanya nayo kazi, anaachana na wakala wake Craig Anderson aliyemuuza kwa tajiri Jackson Motown na kubakwa nchini Afrika Kusini.

Cha kushangaza akiwa ndani ya ndege kubwa ya tajiri aliyetarajiwa kufanya naye kazi, wakikatisha mawingu kwa kasi, Mario Pizaro anamwambia tajiri huyo alitaka kuongea naye na angekuwa ndani ya chumba alichokuwa Catarina dakika tano zilizofuata.

Catarina akabaki akisubiri kwa hamu, moyoni mwake akijua umasikini alikuwa ameuaga, mlango ulipofunguliwa, alishangaa kumwona mwanadamu asiyempenda kuliko wote duniani; Jackson Motown, aliyembaka kwa mara ya kwanza na kuahidi kwamba lazima Catarina angekuwa mke wake atake asitake.

Moyo wa Catarina umeshtuka kupita kiasi kwani Motown ameingia chumbani mwake ndani ya ndege hiyo akiwa uchi wa mnyama, akijua mchezo wa kubakwa ndiyo uliokuwa ukifuata, Catarina anamwonya Motown asidiriki kufanya hivyo kwani siku hiyo asingekubali na kama angekwenda mbele na kumgusa, kiatu chenye kisigino cha chuma alichokishika mkononi kingemharibu Motown uso.

Alichokifanya Motown ni kufungua mlango na kumwita mtu kwa jina la Dragon, kipande cha baba cheusi cha miraba minne kikaingia na kuamuriwa kimkamate Catarina na kumlaza kitandani kisha kumvua nguo zote, Catarina akalia kwani hakuwa na uwezo wa kupambana na Dragon.

Hayo yakitokea ndani ya ndege, nchini Tanzania familia ya Catarina na mchumba wake Kevin wanafuraha mno kwa sababu amepata mkataba wa kwenda kufanya kazi New York, jambo lililokuwa ndoto yake, kwa Kevin anaiona New York akilini mwake akijua muda si mrefu angeitwa kuungana na Catarina, hakuna hata mmoja kati yao anayeelewa yanayompata Catarina ndani ya ndege.
Je, nini kitaendelea?

SONGA NAYO…
Catarina alilia huku akitetemeka mwili mzima kwa hofu baada ya kumsikia Jackson Motown akimwamuru Dragon amvue nguo, hakuwa na uwezo wa kupambana na kipande cha mtu kama kile, alitamani angekuwa na kisu lakini ndani ya chumba alichokuwemo hakukuwa na silaha kama hiyo, silaha pekee aliyoitegemea kujiokoa ni kiatu chake.
Bila huruma Dragon aliruka na kumkamata kwa mikono miwili, kisha kumtupa kitandani, kiatu alichokuwa nacho Catarina kikaruka na kuanguka nyuma ya kitanda, akawa hana silaha tena! Nguo alizovaa mwilini zikachanwa kama magazeti na kujikuta amelala chali akiwa utupu, Dragon amemkandamiza juu ya kitanda.
“Leave me alone, you are so rich and successful! Why be a rapist?”(Niachie, wewe ni tajiri na mtu uliyefanikiwa kwanini uwe mbakaji?)
“I am doing this because you said no!”(Nafanya hivi kwa sababu ulikataa!)
“Please stop, you are hurting me!”(Tafadhali acha, unaniumiza!)
“I can’t stop, till I get what I want!”(Siwezi kuacha mpaka nipate ninachotaka!)
Bila huruma Jackson Motown alimlalia Catarina tumboni na kifuani na kuanza kumwingilia bila ridhaa yake, ilikuwa ni mara ya pili kwa Catarina kubakwa tena na mtu yule yule, kumbukumbu za Kevin zikarejea kichwani mwake, akaichukia kazi ya uanamitindo kwa sababu sasa alikuwa amefahamu yaliyokuwa yakiendelea kwenye ulimwengu huo.
Wakati akilia Jackson Motown aliendelea kumwingilia bila huruma, damu nyingi zikamtoka na kulowanisha mashuka kitandani, haukupita muda mrefu giza likamwigia machoni, akahisi moyo wake unasimama, baadaye hakujua tena kilichoendelea.
“Wake up! Wake up!”(Amka! Amka!) Jackson Motown pamoja na Dragon walianza kumtingisha Catarina baada ya kugundua alikuwa hana fahamu kabisa.
Dragon akakimbia bafuni ambako alichota maji kwenye jagi na kuja kummwagia ili azinduke lakini haikuwezekana, Catarina aliendelea kuwa kimya, walipompapasa kifuani wakagundua moyo wake ulikuwa ukipiga kwa mbali sana, hofu ya kuua ikawaingia.
***
Ahadi ya Catarina kwa wazazi wake ilikuwa ni kupiga simu mara tu akitua New York, ilikuwa ni safari ya saa 9 mpaka kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa JFK Kennedy, wote walikuwa wakihesabu saa na siku hiyo saa moja ilionekana sawa na mwaka mzima, saa 9 zilikuwa ni sawa na miaka 9 ya kusubiri.
Baada ya uvumilivu hatimaye muda huo ukafika, macho na masikio yao yakaelekezwa kwenye simu za mikononi, wakisubiri kengele ilie lakini haikuwa hivyo, saa tano zaidi zikapita na wasiwasi ukaanza kuwaingia. Hatimaye wakafikia uamuzi wa kupiga simu Afrika Kusini kuongea na Craig Anderson ili kufahamu kama labda yeye alikuwa amepigiwa simu ama alikuwa na taarifa zozote za kilichokuwa kikiendelea.
“We have no any information regarding Catarina!”(Hatuna taarifa yoyote juu ya Catarina!)
“Are you sure?”(Una uhakika?)
“Yeah! May be you should call Mario Pizaro!”(Ndiyo! Labda umpigie Mario Pizaro!)
“Who is Mario Pizaro?(Mario Pizaro ni nani?) Mama yake Catarina aliuliza.
“Her new agent in New York!”(Wakala wake mpya hapo New York!)
“Do you have his number?”(Una namba yake?)
“I will send you all his contact details by sms!”(Nitakutumia taarifa zake zote kwa meseji ya simu!)
“Thank you!”(Ahsante!)
Haukupita muda mrefu sana meseji ikaingia kwenye simu ya mama yake Catarina, alipoifungua alikuta ni ya Craig ikiwa na taarifa zote za mawasiliano mpaka jina la kampuni yake la MP Designs na mahali ofisi zilipokuwa! Kabla hajapiga simu iliita, akijua ni ya Catarina aliipokea, akakutana na sauti ya Kevin.
“Mama vipi mmepata mawasiliano yoyote, mimi naanza kuingiwa na wasiwasi, hata masomo hapa chuoni yameanza kunishinda!”
“Bado mwanangu, kila mtu sasa amechanganyikiwa ila nimepata mawasiliano ya wakala wake huko New York, hebu kata simu kwanza nimpigie halafu nitakujulisha!”
Simu ikakatwa, mama yake Catarina akapiga namba ya Mario Pizaro, ikaita bila kupokelewa, akaendelea kufanya hivyo karibu mara ishirini lakini bado simu haikupokelewa! Kitendo cha simu kuita kilionyesha kuwa tayari Mario Pizaro alishawasili New York na kama yeye alishawasili hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Catarina, sasa kwa nini asiwapigie simu? Mama yake alijiuliza bila kupata jibu.
Siku ya kwanza ikapita bila mawasiliano yoyote, mpaka siku tano baadaye hali ilikuwa hiyo hiyo, ikabidi wasiwasi ulipozidi, wazazi wa Catarina wakiwa na Kevin waende Polisi kutoa taarifa ambako walishauriwa waende Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ambako wangewasiliana na waziri pengine angeweza kumtumia Balozi wa Tanzania nchini Marekani kufuatilia uwepo wa Catarina nchini humo.
Walifika ubalozini na kutoa maelezo kwa Balozi ambaye alimwita Mkurugenzi wa Mambo ya Nchi za Nje aliyeshughulika na Marekani, wakaamua kumpigia Balozi huko Washington DC na kumwomba msaada, kila mtu alikuwa tayari kusaidia, kifupi lilishaanza kuwa suala la kitaifa kwa sababu ya umaarufu wa Catarina.
“Nitamtuma mtu kwenda New York kesho, akaitafute hiyo kampuni ya Mario Pizaro Designs mpaka aipate na kumwona huyo Mario Pizaro mwenyewe!” balozi alisema.

Je, nini kitaendelea? Catarina yuko hai? Fuatilia wiki ijayo siku ya Jumatatu katika gazeti la Championi Jumatatu.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply