The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi Maelezo: Serikali Inaitambua Mitandao ya Kijamii

tbn1-1

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali (katikati) Dk. Hassan Abbas, akizungumza jambo wakati akifungua semina hiyo.

tbn1-2

Kaimu Meneja Mwandamizi, Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili, ambaye ni miongoni mwa wadhamini wa semina hiyo kutoka NMB, akizungumza jambo.

tbn1-3

Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi, akizungumza.

tbn1-4

Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale (kushoto) na Joyce Nsekela,wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

tbn1-5

Mmoja wa wanasemina hiyo akichangia mada.

tbn1-6

Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina hiyo.

tbn1-7

Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, akitoa somo katika mafunzo hayo.

tbn1-8

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

SERIKALI imesema kuwa inaitambua mitandao ya kijamii kuwa ni vyombo vya habari kama vingine nchini, na amewaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali.
Hayo ameyasema jana Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, wakati akifungua Semina ya Mwaka na Mafunzo ya Tanzania Bloggers Network (TBN), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema serikali inaitambua mitandao ya kijamii (blogs na websites) kuwa vyombo rasmi vya habari nchini.
Alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti yanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kuelekeza chanzo cha picha hizo tofauti na ilivyo sasa.
Vilevile alitoa rai akisema blogs hazina tofauti na vyombo vingine vya habari hivyo wahusika wa mitandao hiyo wanapaswa kuzingatia sheria na weledi wa kazi zao.
Naye Mwenyekiti wa muda wa mitandao hiyo, Joachim Mushi aliwataka wanamitandao hiyo kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa kero zao na changamoto zinazowakabili ili kuziwasilisha serikalini.
Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto walizonazo walimwambia Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikali ikiwa ni pamoja na kunyimwa ‘Press Cards’, jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi sehemu panapokuwa na viongozi wakuu wa kiserikali.

Comments are closed.