The House of Favourite Newspapers

Mkwasa aita jeshi la kuivaa Nigeria

0

Mkwasa-Stars.jpg

Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa (kushoto).

Said Ally,Dar es Salaam

KOCHA mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa, amewaita jumla ya wachezaji 24 ambao wataunda kikosi cha timu hiyo ambacho kitacheza na Nigeria katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afrika (Afcon) Septemba, mwaka huu.

Mkwasa ameita kikosi hicho kwa ajili ya kukamilisha ratiba ya Kundi G ambapo hata kama Stars itashinda haitasonga mbele kwa kuwa tayari Misri imeshafuzu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkwasa alisema kuwa licha ya kuwa mchezo huo hauna faida yoyote kwao, watajituma kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwa ajili ya kusaka nafasi ya kupanda katika viwango vya ubora duniani.

“Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo, tuna lengo la kushinda ili tuweze kujisogeza kwenye viwango vya ubora vya dunia ambapo kama tukishinda nchini Nigeria tutaongeza alama nyingi.

“Mara baada ya kuwaita wachezaji hawa watakuwa na kambi fupi itakayoanza mwezi ujao na kudumu kwa siku tano kabla ya kuivunja kwa sababu hiki ni kipindi timu nyingi zipo kwenye maandalizi, hivyo kuwapata wachezaji inakuwa ngumu kidogo.

“Lakini wachezaji hawa siyo ambao nitaenda kuwatumia Nigeria kwa sababu tutaendelea kuwafuatilia kwenye ligi na endapo mtu atashuka kiwango tutamuacha,” alisema Mkwasa.

Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji Deogratius Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya (Yanga), Aishi Manula (Azam), Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ (Simba), Aggrey Morris na Erasto Nyoni (Azam).

Wengine ni Himid Mao, Farid Mussa wa Azam, Mohammed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude (Simba), Hassan Kabunda (Mwadui), Rajab Ibrahim ‘Jeba’ (Mtibwa) na Juma Mahadhi (Yanga).

Mkwasa aliongeza kuwa kikosi kitakuwa na washambuliaji Simon Msuva (Yanga), Joseph Mahundi (Mbeya City), Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam) na Jeremiah Juma (Prisons).

Leave A Reply