The House of Favourite Newspapers

Mpambano Mkali… Waasi 80 Wauawa Congo

0

JESHI la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema, limewauwa waasi zaidi ya 80 wa ADF Nalu Wilayani Beni, katika operesheni dhidi ya makundi ya waasi.

 

Hii ni operesheni inayokuja, baada ya waasi hao kuendelea kutekeleza mauaji ya raia zaidi ya 100 tangu mwezi Novemba, katika Wilaya hiyo na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa wakaazi wa Beni.

Wananchi Mashariki mwa nchi hiyo wameendelea kuandamana kulaani utovu wa usalama, wakishinikiza kuondoka kwa Jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachosema, limeshindwa kuwalinda.

Katika wii za hivi karibuni, Beni ilikumbwa na matukio mablimbali hasa, mauaji ya raia, ambapo kundi la waasi wa Uganda la ADF lilishtumiwa kuhusika na mauaji hayo ya kikatili.

Leave A Reply