The House of Favourite Newspapers

Mpoto awachana wasanii kukimbilia Nigeria, Sauz

0

Mrisho Mpoto akisikiliza moja ya maswali kutoka kwa mtangazaji wa Global TV. 

Mrisho Mpoto akijibu moja ya maswali.

Mtangazaji wa Global TV Online, Shovienly (Kushoto) akifanya mahojiano na Mrisho Mpoto.

Mrisho Mpoto akiwa katika pozi mara baada ya mahojiano na Global TV Online.

Mrisho Mpoto akisalimiana na Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

Kutoka kushoto, Elvan Stambuli, Mrisho Mpoto pamoja na Walusanga Ndaki.

Mrisho Mpoto akiwa na Gabriel Ng’osha,

Mrisho Mpoto akiwa na Shafii Mohamed wa kitengo cha IT.

Mrisho Mpoto pamoja na Edwin Lindege wa kiyengo cha IT.

STAA wa nyimbo za Asili, Mrisho Mpoto leo mchana alitinga ndani ya Jengo la Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na kipindi cha Global TV Online ambapo alifunguka mengi ikiwa ni pamoja na kuwachana wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanaokimbilia nchini Afrika Kusini na Nigeria kwa kudhani huko kuna mafanikio zaidi.

Akizungumza katika Kipindi cha Mtu Kati, kinachoruka hewani na Global TV, Mrisho alisema kwua anachukizwa zaidi na jinsi wasanii wanaokimbilia nje ya nchi kutengeneza nyimbo na video.

“Huwezi kunikuta nakimbilia kutengeneza video nchini Nigeria, Sauz eti kisa kupata mafanikio. Wasanii wanatakiwa kutambua kuwa muziki wetu unahitaji kwanza ubadilike nchini.

“Wasanii tunakosa ladha ya kuutambulisha muziki wetu. Huwa najivunia sana ninapoenda Ulaya wazungu wengi wananitambua na kujaa kwa wingi kushuhudia shoo yangu. Lakini wasanii wenzetu wakienda Ulaya huko wanaenda kukutana na Watanzania wanaoishi huo na siyo wazungu na hata shoo zao wanaenda kuwapigia mashabiki wn=engiw aliokimbilia huko.”

Mahojiano kamili yatapatika kupitia Global TV Online kuanzia wiki ijayo.

(PICHA, STORI: ANDREW CARLOS)

Leave A Reply