The House of Favourite Newspapers

Mrema Awataka Mahakimu Kuwa Makini na Hukumu za Watumia ‘Unga’

0

1Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema akizungumza na wanahabari.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole nchini, Augustino Mrema amewataka mahakimu kuwa makini na hukumu ambazo wanatoa kwa watumiaji wa madawa ya kulevya ‘mateja’ wanapowahukumu kwenda gerezani na badala yake wapate vifungo vya nje ili wapate tiba.

2.Mkutano ukiendelea.Mkutano ukiendelea.

Hayo ameyasema leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari.

“Watumiaji wa madawa ya kulevya wasipelekwe magerezani bali wapelekwe kwenye vituo vya tiba vya Muhimbili, Temeke na Mwananyamala ili waanze kupata tiba,” alisema Mrema.

3.Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Vilevile aliliomba jeshi la polisi kuwaondoa Polisi Jamii katika maeneo yote kwa madai kuwa amebaini watu hao wamekuwa wakiwakamata wahanga wa madawa ya kulevya kwa nia ya kutaka kupewa rushwa na siyo kutimiza majukumu yao.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply