Mshindi wa Gari la SportPesa Asimulia Alivyoshinda

PROMOSHENI ya Faidika na Jero iliyokuwa inachezeshwa na Kampuni ya kubashiri ya SportPesa imemalizika kwa Yusuph Jackson, 29, mkazi wa Serengeti kujishindia zawadi ya gari jipya aina ya Renault KWID.

 

Promosheni hiyo ilidumu kwa siku 40 ambayo tofauti na zawadi ya gari hilo jipya, washindi mbalimbali walikuwa wakipatikana kwa kila siku wakijishindia simu janja aina ya Samsung A10s. Yusuph amesimulia jinsi alivyoshinda gari hilo;

 

Kumbe alitumia siku 20 tu kushinda gari

“Wakati ninaanza kucheza na SportPesa sikuwa nafahamu kuhusu michezo hiyo ya kubashiri kutokana na mambo ya kazi kunibana, kutokana na mwingiliano huo baada ya kuona matangazo kupitia Televisheni kwamba kuna Promosheni ya Faidika na Jero kutoka Tigo, nikaamua kujiunga na SportPesa kubashiri.

 

“Na hazikupita siku nyingi tangu nilipoanza kucheza na SportPesa ikielekea siku ya hitimisho ya siku 40 ambayo ilikuwa siku ya kilele cha kubashiri na mshindi wa gari anapatikana.

“Mimi nilicheza kama siku 20 hivi promosheni hiyo ikielekea kumalizika na ndiyo nikapigiwa simu na SportPesa nikapewa taarifa za kushinda gari hili jipya nililozawadiwa aina ya Renault KWID.

 

Baada ya gari, apiga hesabu za nyumba

“Natamani familia yangu kuishi vizuri kwa kupata sehemu nzuri ya kulala, nashukuru tayari nimepata gari, hivyo hivi sasa natamani niwe na nyumba yangu ya kulala.

Awaaminisha Watanzania kuwa hakupangwa kuwa mshindi

“Niwaaminishe Watanzania, pia wakazi wenzangu wa Serengeti kuwa hii zawadi ya gari niliyoipata haikupangwa, imetokana na juhudi zangu za kucheza zaidi na SportPesa hadi kufanikiwa kushinda zawadi, kingine kikubwa mimi hakuna mtu ninayejuana naye kwenye kampuni hiyo.”

 

Mke wake naye atia neno

“Mimi alinipigia simu ya ushindi wake wa gari akiwa kazini, lakini sikuamini sana, lakini wakati ananiambia hivyo yeye mwenyewe alikuwa na wasiwasi akijua huenda wakawa matapeli, lakini akaniambia tusubirie utaratibu utakuwaje.

 

“Alivyorudi jioni alinionyesha taarifa rasmi ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi na tayari SportPesa wameniomba majina na namba zangu za simu ambazo tayari nimewatumia, siku inayofuata akanipigia simu nimuandalie nguo ili aende kufuata hilo gari ndiyo nikaamini.”

 

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment