The House of Favourite Newspapers

Mtoto Mchanga ‘Azaliwa’ Mara Mbili

_92078519_61110f85-9584-48ea-b0e8-b0d3f5bf29a9MTOTO mchanga wa kike kutoka Lewisville, Texas, ‘amezaliwa’ mara mbili baada ya kutolewa katika kizazi cha mama yake kwa dakika 20 ili kufanyiwa upasuaji.

Akiwa na ujauzito wa miezi minne, Margaret Hawkins Boemer aligundua kuwa binti yake, Lynlee Hope, ana uvimbe katika uti wake wa mgongo.

_92070888_boemers4Uvimbe huo unoajulikana kama sacrococcygeal teratoma, ulikuwa unasukuma damu kutoka kwa mtoto huo, jambo lililoongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo kutofanya kazi.

Baby Lynlee alikuwana uzito wa chini ya kilo moja wakati wapasuaji walipomtoa kwenye uzao wa mamake.

Bi Boemer awali alikuwa amebeba mimba ya pacha, lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya kumaliza miezi mitatu ya kwanza. Awali alishauriwa kuitoa mimba hiyo kabla ya madakatari wa wa hospitali ya watoto ya Texas Children’s Fetal Center kumpndekezea upasuaji huo wa hatari.

Uzito wa uvimbe huo na ule wa mtoto ulikuwa karibu sawa wakati upasuaji ulipofanywa. Aliarifiwa kuwa mwanawe Lynlee ana asilimia 50 ya kufanikiwa kuishi.

Bi Boemer aliambia CNN: ” nikiwa na miezi mitano, uvimbe huo ulikuwa unasitisha moyo wake kufanya kazi, kwahivyo ilikuwa ni uamuzi baina ya kuruhusu uvimbe huo ummalize au kumpa nafasi ya kuishi.

“Ulikuwa uamuzi wa rahisi kwetu: Tulikuwa tunataka kumpa maisha.”

‘Moyo wake ulisiti kupiga’

Upasuaji

Daktari Darrell Cass wa Texas Children’s Fetal Centre nimojawapo ya matabibu waliotekeleza upasuaji huo. Amesema uvimbe huo ulikuwa mkubwa, kiasi cha kuhitaji upasuaji mkubwa kuufikia, jambo lililohatarisha maisha ya mtoto huyo.

Moyo wa Lynlee nusra usite kupiga wakati wa upasuaji huo lakini mtaalamu wa moyo alimsaidia kuendelea kuishi wakati uvimbe huo ulipakuwa unatolea, aliongeza.

Madaktari hao baadaye walimrudisha katika uzao wa mamake na kuufunga uzao kwa kuushona.

Bi Boemer alisalia kitandani kwa wiki 12 zilizofuata, na Lynlee alizaliwa kwa mara ya pili mnamo Juni 6.

Alizaliwa kwa upasuaji akiwa aribu kutumiza miezi tisa tumbano, na alikuwa na karibu kilo mbili na nusu.

Lynlee alipofikisha siku nane baada ya kuzaliwa, alifanyiwa upasuaji mwingine kutoa uvimbe uliosalia katika uti wake wa mgongo.

Dr Cass anasema mtoto huyo sasa amerudi nyumbani na anaendelea vizuri.

“Bado ni mchanga lakini anaendelea vizuri,” amethibitisha.

Sacrococcygeal teratoma ni uvimbe usiojitokeza sana na huwapata watoto 30,000 kati ya 70,000 wanaozaliwa.

Haijulikani husababishwa na nini lakini watoto wa kike huathirika mara nne zaidi kuliko wavulana.

 

TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.