The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Rais Ateuliwa Kuwa Msaidizi wa Rais

0

MTOTO mkubwa wa kiume wa Rais Ali Bongo wa Gabon, Noureddin Bongo Valentin ameteuliwa kuwa mratibu wa masuala yote ya Rais.

Noureddin ameteuliwa katika nafasi hiyo ili kumsaidia Rais katika masuala yote ya kitaifa. Nafasi hiyo ya mratibu wa shughuli zote za Rais ilitengenezwa baada ya kumalizika kikao cha baraza la washauri na kutolewa taarifa rasmi na msemaji wa serikali, Edgar Miyakou.

Hii inamaanisha Noureddin Bongo atakuwa mshirika wa karibu sana wa baba yake, Ali Bongo, ambaye aliingia madarakani mwaka 2009. Mara baada ya kifo cha baba yake, Omar Bongo Ondimba aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 42.

Leave A Reply