The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo Usijimwambafai Kupitiliza

0

USIKU wa Ijumaa ya wikiendi iliopita naamini ulikuwa mzuri kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini baada ya bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo kumshinda kwa pointi, Arnel Tinampay raia wa Filipino.

 

Mwakinyo alishinda pambano hilo la raundi kumi, uzito wa Super Welter ambalo halikuwa la ubingwa kwa pointi na kupelekea mzozo mkubwa kutoka kwa mashabiki kutokana na kuwepo ambao waliamini amepigwa na wengine ameshinda.

 

Mjadala ulikuwa mkubwa  katika kila eneo nchini hali iliyopelekea niamini mchezo wa ngumi  unapendwa nchini lakini kutokana na kuwa na mazingira rafi ki umekuwa ukionekana wa kihuni.

Lakini hali ilichafuka baada ya bondia huyo kutamka waziwazi  kupitia sauti yake iliokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii akimtupia lawama nzito bondia mstaafu Rashid Matumla ‘Snake Man’.

 

Huenda Mwakinyo hakuwa anamjua vizuri Matumla kutokana na shutuma alizokuwa anazitoa kwa kuwa ni mmoja ya watu walifi kisha mchezo huo hapo ulipo kutokana na heshima kubwa alioipa nchi. Lakini shida yangu hapa siyo Matumla kwa kuwa yeye alishamaliza na anapaswa kupewa heshima yake kama ilivyokuwa zamani haijalishi nini alikiongea kwa kuwa yeye ni mchambuzi na itabaki kuwa hivyo.

 

Mwakinyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 17, akishinda 15  kati ya hayo 11 ni kwa KO huku akipigwa mara mbili na moja ikiwa  kwa KO, alikosea kwa kauli yake licha ya kuomba msamaha na kukosea tena.

 

Hapa nimekuwa nikijiuliza nani yupo nyuma yake, nani anamueleza mipaka yake ya kuzungumza na nini cha kuzungumza tena kwa wakati gani au kwa nini azungumze.

 

Kosa la kwanza analolifanya Mwakinyo kwa sasa ni kujibizana na mashabiki kwa kuamini hawezi kukosolewa kwa kuwa yeye ni bondia na anahisi hawezi kukosea. Mwakinyo anatumia muda mwingi kujaribu kuwaelewesha watu wasiojua ngumi kama alishinda kihalali huko katika mitandao ya kijamii kuacha kuangalia mambo yake ya msingi ambayo kwa ajili ya mapambano yake mengine.

Hivi umewahi kumuona bondia bora duniani, Flody Mayweather akipigizana kelele na mashabiki  au wachambuzi juu ya kiwango chake ulingoni kama anabebwa au vipi. Sisi  kwenye soka watu wanatukanwa matusi mazito lakini huwasikii wakipigizana kelele au kwa kuwa eti kocha amepewa ushauri ambao kwake pengine aliona mbovu.

 

 

Baada ya kukosea anakuja kuomba msamaha tena kwa lugha nyepesi kwa watu ambao wamemuunga mkono kwenye pambano lake tena akiwa amezungukwa na watu kibao nyuma yake. Nini maana ya viongozi basi ameshindwa kujifunza hata kupitia nyota wa kimataifa Mtanzania, Mbwana Samatta alipokosolewa na alikiri na kuahidi kubadilika, kwa nini Mwakinyo ameruhusu kuingia kwenye mtego ambao huenda ukampoteza kirahisi?

 

Naamini Tanga ina watu wazuri na wenyewe hekima kubwa lakini bado anajuliza nao walikuwa wapi kumuongoza bondia wetu ambaye tunaamini ataifanyia makubwa nchi wanamuacha apotee katika kundi la wanywaji wa kahawa ya kijiweni.

 

Ushindi wa siku moja ambao umeiletea sifa nchi, usimfanye akajimbwafayi kupitiliza kiasi kwa kuwa  bado safari yake kwenye ngumi bado ndefu inayohitaji washauri ili kufi kia ndoto zake.

 

Lakini anapaswa kuelewa sikwamba wanamsema kama wanamchukia au hawampendi isipokuwa wanataka afanikiwe zaidi katika mchezo wa ngumi kama ilivyokuwa kwa waliomtangulia.

 

Sijui kwamba anatambua muda gani ametumia kuutafuta kubwa aliokuwa nao sasa kupitia wadhamini wanamsapoti ambao ni rahisi kupotea kutokana na kuingia kwenye rekodi mbovu kwa wadhamini wake. Mara kadhaa katika ngumi wanaomba wadhamini kupitia makampuni kujitokeza sasa kuweka kwenye mchezo huo sasa Mwakinyo hakufi kiria ukubwa wa kauli zake utakuwa na hasara gani kwenye tasnia ya mchezo huo kiujumla.

 

Naamini Mwakinyo ni mmoja kati ya mabondia wenye uelewa na busara lakini hapaswi kukubali kutumiwa kwa kujimwambafayi kupitia watu wanaomzunguka  kwa ushauri wa hovyo wanampatia.

 

Mwakinyo anachotakuwa kujua mashabiki wanataka ngumi, aache mikono ifanye kazi yake asikubali kutumia mdomo na mikono yake kujibizana  katika mitandao haiwezi kumletea faida zaidi kumjengea chuki kwa watu ambao tunapenda kuona akifi ka mbali. Najua pengine aliamua kujibu kisha kukiri makosa kwa kauli hovyo pengine baada ya kushauriwa na wakubwa lakini sina hakika kama alikaa chini nakurejea pambano zima kwa kusikiliza ushauri alitakiwa kuufanyia kazi.

MAKALA: IBRAHIM MUSSA, PICHA: RICHARD BUKOS

UWOYA – “WEMA na AUNT Mmh, Ku KISS MDOMONI, Nakula BATA Kama KAWAIDA”

Leave A Reply