The House of Favourite Newspapers

Mwakyembe Azindua Mashindano ya Shimmuta Mwanza

0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini, Dkt. Harrison Mwakyembe leo Jumamosi, Novemba 30, 2019 amezindua mashindano ya Shirikisho la Mmichezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafasi Tanzania (SHIMMUTA) katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mwakyembe amewapongeza viongozi wa Shimmuta kwa kuleta timu 46 ambapo zitashiriki michezo 12 ya Shimmuta.

“Nawapongeza sana viongozi wa Shimmuta kwa kuleta timu Mwanza katika mashindano haya, pia nawaomba wachezaji mliofika mcheze kwa amani ili mashindano haya yaweze kufana,” amesema Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe ameeleza masikitiko yake kwa Mkoa wa Mwanza kutotoa mapokezi stahiki kwa mashindano hayo.

“Mashindano ya Shimmuta ni mashindano makubwa, lakini nimeshangaa kuona Mwanza hawajaandaa mapokezi yoyote, nafikiri tutatafuta mikoa ingine ambayo inao uhitaji kwani kuja kwa timu hizi kumeongeza kipato kwa wakazi wa Mwanza kwa kua hoteli zimejaa mpaka sasa,” aliongeza Waziri huyo.

NA JONHSON JAMES | GPL, MWANZA

Leave A Reply