Mwanahabari Makongoro Oging’ Azikwa Tarime
Mke wa Makongoro, Naza Oging’ akimuaga mumewe kwa simanzi nzito.
Mama mzazi wa marehemu aitwaye Magreth Oging’ akimuaga mwanaye kwa majonzi.
Mtoto wa kwanza wa marehemu, Leah Makongoro akimuaga baba yake.
Mdogo wa marehemu aitwaye Juma Oging’ akimuaga kaka yake.
Dada wa marehemu akimuaga kaka yake kwa simanzi.
Hilaly Daud akiweka udongo kwenye kaburi la Makongoro Oging’.
Kaka wa marehemu aitwaye Nelson Oging’ akiweka udongo kwenye kaburi la mdogo wake.
Kaka wa marehemu wakifarijiana.
Kaka wa marehemu aitwaye Nelson Oging’ akiweka shada la maua kwenye kaburi la mdogo wake.
Madada wa marehemu Makongoro wakiweka mashada kaburini.
Ofisa Utawala wa Global Publishers, Soud Kivea akiweka shada la maua kwa niaba ya wafanyakazi wa Global kwenye kaburi la Makongoro Oging’.
Magreth Oging’ akiwa na simanzi nzito.
Kaka wa marehemu aitwaye George Oging’ akimfariji Magreth Oging’.
Mama wa marehemu Magreth Oging’ na mke wa marehemu Naza Oging’ wakilia kwa uchungu.
Magreth Oging’ akiweka shada kwenye kaburi la mwanaye.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul akiweka udongo kwenye kaburi la Makongoro.
Naza Oging’ akiweka shada kwenye kaburi la mumewe.
Leah na Naza wakilia kwa huzuni.
Naza akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe.
Leah Makongoro akiweka udongo.
Mtoto wa Makongoro, Yohana Makongoro akilia kwa simanzi nzito.
Mwandishi Mwandamizi na Mpiga Picha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos (katikati) akiweka udongo kwenye kaburi la Makongoro.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa mbele ya waombolezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (mwenye miwani) akisaidiana na waombolezaji kupeleka jeneza la Makongoro kaburini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa mbele ya kaburi la Makongoro.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua.
MAZIKO ya aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Makongoro Oging’ yamefanyika jana nyumbani kwao katika Kijiji cha Marasibora wilayani Tarime mkoani Mara.
Makongoro Oging’ aliaga dunia jioni ya Mei 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kuagwa juzi Mei 26 katika hospitali ya Amana, Ilala ambapo siku hiyo hiyo mchana, safari ya kuusafirisha mwili wake kuelekea kijijini kwao Marasibora, Tarime ilianza.
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL – MARASIBORA, TARIME