The House of Favourite Newspapers

Mzungu Amvaa Kocha Mpya Simba

0
Mtendaji Mkuu wa Klabu Simba, Senzo Mazingisa.

 

WAKATI Simba ikitarajiwa kumtambulisha kocha wake mkuu leo, taarifa zinasema kuwa kumekuwa na vita kubwa kati ya Beston Chambeshi na Mzungu mmoja.

Mpaka jana asubuhi, Chambeshi ndiye alikuwa anatajwa kuwa ameshamalizana kila kitu na Simba na leo angetambulishwa, lakini taarifa za jana zimesema kuwa juzi, uongozi wa timu hiyo ulifanya mazungumzo na kocha Mzungu kutoka Uingereza.

 

Simba ambayo imeshamalizana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola, inatarajiwa kumtambulisha kocha mkuu leo na jioni atakuwa mazoezini.

Beston Chambeshi.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo ambayo inawania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara imesema kuwa Chambeshi ambaye hadi jana ndiyo alikuwa anaaminika atachukua nafasi hiyo iliyoachwa na Patrick Aussems ambaye ametimuliwa kwenye timu hiyo amekumbana na upinzani.

 

“Kuna Mzungu mmoja alikuja juzi, bado sijapata jina lake kwa kuwa imekuwa siri kubwa na wanafahamu watu wawili tu C.E.O, Senzo Mazingisa pamoja na Mwenyekiti Mohammed Dewji.

 

“Lakini jamaa alifanya mazungumzo juzi na jana na inavyoonekana anaweza kumpa upinzani mkali Chambeshi kama hatapunguza baadhi ya vitu ingawa bado anaonekana kuwa kwenye nafasi.

 

“Kama alivyosema Mo leo ndiyo, timu hiyo itamtambulisha kocha wake mkuu, hivyo ni jambo la kusubiri tuone,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Stori na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Leave A Reply